Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Featured Posts

Friday, February 8, 2019

Unakumbuka lile boti la Plastiki kutoka Lamu?


Boti la kwanza lililotengenzwa kwa taka za plastiki huko Lamu Kenya limefika visiwani Zanzibar. Boti hili liliundwa katika jitihada za kukabiliana na tatizo la taka za plastiki zilizojaa katika ufukwe wa bahari Lamu pwani ya Kenya. Tulikutana na mabaharia wake mwaka mmoja tangu tulipoangazia kuanza kwa ujenzi wake...

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 08.02.2019: Rashford, Ginter, Kante, Mourinho, Coutinho, Grimaldo, Rugani

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, yupo katika mazungumzo ya kina kuhusu kuimarisha mkataba wake ambao huenda ikachangia kuongezwa kwa mshahara wake kwa zaidi ya mara mbili na mkubaliano ya thamani ya £200,000 kwa wiki katika mkataba wa muda mrefu(Star)
Tottenham na Arsenal wanamuangalia beki wa kati wa Borussia Monchengladbach kutoka Ujerumani Matthias Ginter, mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports)
Huenda Paris St-Germain ikatafuta kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27, katika msimu w a joto. (Le10 Sport, kupitia Sun)

Mbunge Jackline Ngonyani ataka wabunge ambao hawakutahiriwa wakaguliwe Tanzania

Kumekuwa na mjadala nchini Tanzania na zaidi katika mitandao ya kijamii baada ya mbunge mmoja kulishauri bunge kuweka utaratibu maalum kukagua wanaume walio na 'mkono sweta' au wanaume ambao hawajatahiriwa.
Mbunge maalum Jackline Ngonyani amependekeza hatua hiyo katika hoja ya kujadili udhibiti wa maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.
Akizungumza bungeni, Mbunge huyo ameeleza bunge kwamba lengo la 90-90-90 la virusi vya ukimwi litafikiwa nchini Tanzania, pale kutakuwa na ridhaa ya watu kujipima wenyewe.

Ofisi Ya Rais-Utumishi Yafanya Ufuatiliaji Wa Utekelezaji Wa Waraka Wa Mavazi Kwa Watumishi Wake


Idara ya Ukuzaji  Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo, imefanya ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na kiwango cha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kuhimiza watumishi wa umma nchini kuzingatia waraka huo mahala pa kazi.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao unawaelekeza watumishi wa umma aina ya mavazi wanayostahili kuyavaa mahala pa kazi.

Bibi Mishinga amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi ni msimamizi wa miongozo mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambapo kanuni ya kwanza inaelekeza utoaji wa huduma bora na kuongeza kuwa moja ya kigezo cha watumishi wa umma kutoa huduma bora ni pamoja na kuvaa mavazi  yenye staha.

Bibi Mishinga amefafanua kuwa, zoezi hilo la ukaguzi katika ofisi ya Rais-Utumishi limebaini kuwa asilimia 95 ya watumishi wameonekana kutekeleza vema waraka huo wa mavazi ikiwemo kuwahi kazini na asilimia tano ya watumishi waliobainika kutotekeleza waraka huo wamekumbushwa kuuzingatia.

Aidha, Bibi Mishinga ametoa wito kwa wasimamizi wa taasisi zote za umma nchini  kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa waraka huo na kuwahimiza watumishi walio chini yao  kuwahi kazini kwa ili kutoa huduma bora na kwa wakati kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyohimiza.

Bibi Mishinga  amesisitiza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  ikiwa ndio msimamizi wa waraka huo wa mavazi itaendelea kufanya ukaguzi na ufuatiliaji  katika taasisi zote za umma nchini na haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wa umma watakaobainika kuukiuka.

Thursday, February 7, 2019

BWANA MMOJA MAREKANI AUA SIMBA ALIYEMVAMIA MBUGANI




Mountain lion
Mashambulizi ya Simba  ya nadra nchini Marekani.
Bwana mmoja nchini Marekani amemuua Simba wa milimani ambaye alimshambulia ghafla mbugani.
Simba huyo dume alimvamia kwa nyuma bwana huyo ambaye hakutajwa jina lake katika Hifadhi ya Wanyama ya Colorado.
Maafisa wanyamapori wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Jumatatu ambapo mwanaume huyo amepata majeraha makubwa usoni na kwenye kiganja cha mkono

Monday, May 19, 2014

HUYU NDIE MBU ANAYESABABISHA UGONJWA WA DENGUE

Culicidae,Mbu huyo asili yake ni Afrika lakini hivi sasa amesambaa sehemu mbalimbali duniani hasa sehemu za tropiko na anapatikana majira yote ya mwaka hasa sehemu zenye maji maji. Machapisho mbalimbali ya kimataifa ya utafiti wa kisayansi kuhusu mbu huyo yanaeleza kuwa amekuwepo kwa zaidi ya miaka milioni 150 iliyopita na kusabisha maradhi kwa binadamu wa kale.
Utafiti wa awali uliofanywa na mwanasayansi Fredric Hasselquist mwaka 1757 ulitaja mbu huyo kwa jina la Culex aegypti. Jina la Aedes aegypti lilianza kutumika mwaka 1920 na lilianzishwa na mwanasayansi Harrison Gray Dyar, Jr. Aedes ni mbu anayeeneza virusi vinavyosababisha ugonjwa maarufu kwa jina na chikungunya, homa ya manjano na homa ya dengue ambayo hivi sasa inaenea kwa kasi katika jiji la Dar es Salaam.