Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Monday, May 19, 2014

HUYU NDIE MBU ANAYESABABISHA UGONJWA WA DENGUE

Culicidae,Mbu huyo asili yake ni Afrika lakini hivi sasa amesambaa sehemu mbalimbali duniani hasa sehemu za tropiko na anapatikana majira yote ya mwaka hasa sehemu zenye maji maji. Machapisho mbalimbali ya kimataifa ya utafiti wa kisayansi kuhusu mbu huyo yanaeleza kuwa amekuwepo kwa zaidi ya miaka milioni 150 iliyopita na kusabisha maradhi kwa binadamu wa kale.
Utafiti wa awali uliofanywa na mwanasayansi Fredric Hasselquist mwaka 1757 ulitaja mbu huyo kwa jina la Culex aegypti. Jina la Aedes aegypti lilianza kutumika mwaka 1920 na lilianzishwa na mwanasayansi Harrison Gray Dyar, Jr. Aedes ni mbu anayeeneza virusi vinavyosababisha ugonjwa maarufu kwa jina na chikungunya, homa ya manjano na homa ya dengue ambayo hivi sasa inaenea kwa kasi katika jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment