Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, October 24, 2013

Rais Jakaya Kikwete Alipowasili Mjini Dodoma Jana Jioni.



Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye ndege, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma jioni hii, kwa ajili ya kufunga semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa inayomalizika leo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete baada ya kuwasili mjini Dodoma

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma jana jioni

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Uwanja wa Ndege mjini Dodoma baada ya kuwasili jana jioni

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimwongoza Rais Kikwete kwenda eneo la mapumziko baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa

Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki, Uwanja wa Ndege wa Dodoma Jana jioni

No comments:

Post a Comment