Afisaa mkuu msimamizi wa
hospitali ya kijeshi ya Juba, Brigedia Gen Dr Ajak Bullen,ameambia
shirika la redio la Miraya mjini Juba kuwa wanajeshi 66 wameuawa katika
mapigano ya siku mbili.
Watafanyiwa mazishi ya pamoja.
Wakati huohuo afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa raia 26 wameuawa katika mapigano ya siku mbili mjini Juba.
Zaidi ya watu miamoja wamejeruhiwa huku maafisa
wakuu wakijaribu kudhibiti mji huo kufuatia kile ambacho serikali
ilisema ni jaribio la mapinduzi mbalo liliweza kutibuliwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba
Marial Benjamin amesema kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wanajeshi
watiifu kwa Riek Machar aliyekuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir
anayedaiwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi.
Taarifa zinasema kuwa milio ya risasi ingali inasikika mjini Juba.
No comments:
Post a Comment