Maelfu ya watu nchini Tunisia
wamekuwa wakifanya maandamano mjini Sidi Bouzid, kitovu cha harakati za
mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa Rais Zine
el-Abidine Ben Ali miaka mitatu iliyopita.
Waandamanaji wanalalamikia ukosefu wa serikali kupiga hatua za kuridhisha tangu mapinduzi ya kiraia kufanyika.
Mji wa Sidi Bouzid ndiko kijana mmoja mchuuzi
Mohamed Bouazizi alijiteketeza miaka mitatu iliyopita kuonyesha ghadhabu
kwa ambavyo serikali ilikuwa inawanyanyasa raia wake.
Maandamano yaliyofuata tukio la kijana huyo
kujiua, yalimwondoa mamlakani aliyekuwa Rais Zine el-Abidine Ben Ali na
kuchochea maandamano mengine kama hayo katika nchi za kiarabu.
No comments:
Post a Comment