Mh. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi.Fatma S. Ally
Mkuu
wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma S. Ally Ameipongeza kampuni ya simu
ya Airtel kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari
ITISO. Mkuu huyo amesema hayo wakati akitoa hotuba yake katika Mahafali
ya Kidato cha nne iliyofanyika Shule ya Sekondari ITISO Tarehe
18/10/2013 " Nimefurahi kusikia juhudi zilizo onyeshwa na Kampuni, ya
simu ya Airtel kwa kutoa vitabu vya sayansi katika shule hii,hivyo
nichukue fursa hii kwa upekee kuipongeza kampuni hii ya simu" Alisema
Bi. Fatma.
Katika
hatua nyingine aliwataka wanafunzi wa kidato cha nne kujikita zaidi
katika maadalizi ya mitihani iliyoko mbele yao na kuongeza kuwa bado
wanayo nafasi ya kupitia vyema kile walicho kisoma ili waweze kuwa
katika hali nzuri ya kujibu mitihani yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Chamwino Mh. Joel Mwaka alisema wazazi bado wanayo nafasi kubwa kuhakikisha watoto wao wanafanya vema katika masomo yao kwa maana ya kufatilia kwa ukaribu maendeleo yao kitaaluma.Jukumu la ufaulu kwa mwanafunzi linahusisha Mwanafunzi mwenyewe,Mwalimu pamoja na Mzazi,Alisema Bw. Joel
Mkuu wa Shule ya Sekondari Itiso Bw. Andrea A. Mauki Akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Nne wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Mkuu wa Shule ya ITISO Akikabidhi Risala kwa Mgeni Rasmi
Mwenyekiti wa Kijiji cha ITISO akizungumza wakati wa mahafali hiyo.
Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Chamwino Bi.Nyemo Masimba
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya ITISO Bw. Andrea A. Maukia kifuatilia kwa umakini Matukio mbalimbali katika Mahafali hayo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM (Wilaya ya Chamwino) Mh. Joel Mwaka
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Ndugu Raymond Mwakifamba akizungumza katika mahafali hayo
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Ndugu Raymond Mwakifamba akizungumza katika mahafali hayo
Chereko na shangwe kwa Wahitimu...!!!!!
No comments:
Post a Comment