Mazishi ya Nelson Mandela
yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na
kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika mwendazake Nelson
Mandela.
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa
wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale
na mambo ya kisasa.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa
mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya
mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa
anazikwa.
Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela
wa Thembu.
Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa
heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya
kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela
alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu
ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu
la kuendeleza sera zake na urithi wake.
No comments:
Post a Comment