Leo ndio siku ya mazishi ya Mwana wa Mama Afrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Anazikwa kijijini kwao Qunu.
Mandela anayetoka kwenye kabila la
Xhosa alizaliwa Julai 18, 1918 kijijini Mvezo, kando ya mto Mbashe,
Wilaya ya Umtata, Makao Makuu ya Jimbo la Transkei.
Ukoo wa Mandela una mahusiano na Ukoo
wa Kifalme wa Thembu. Baba yake Mandela, Gadla Henry Mphakanyiswa
alikuwa Chifu kwa damu na kwa desturi. Naye akathibitishwa kuwa Chifu wa
Mvezo na Mfalme wa himaya ya Thembu.
Mandela mwenyewe alizaliwa na jina
Rolihlahla, ikiwa na maana ' Mwenye kuvuta matawi ya miti'. Na kwa lugha
yao ina maana ya ' Msumbufu'.
Na hakika, Mandela amekuwa ' Msumbufu' kwa utawala wa kibaguzi hadi pale waliposalimu amri.
Mandela anasimulia, kuwa kumekuwa na
hekaya sizizo za kweli kwenye kabila lao, kuwa naye ( Mandela) alikuwa
mmojawapo katika mlolongo wa kurithishwa Uchifu kwenye himaya ya Thembu.
Kwamba ingefika wakati naye Mandela angetawazwa kuwa Chifu. Mandela
analikanusha hilo, anasema;(P.T)
" Although I was a member of the royal
household, I was not among the privileged few who were trained for
rule. Instead, as a descendant of the Ixhiba house, I was groomed, like
my father before me, to counsel the rulers of the tribe."( Long Walk to
Freedom, pg.5)
Kwamba ingawa alizaliwa katika ukoo wa
Kichifu, lakini, hakuwa mmoja waliokuwa na fursa ya kupata mafunzo ya
kuwa watawala.
Lakini, kwa vile ana chimbuko la koo la Ixhiba,
aliandaliwa, kama baba yake, kuwa mshauri wa watawala wa kabila lao.
Mandela anasimulia, kuwa katika miaka
ya baadae ya utotoni, alibaini, kuwa baba yake hakuwa tu mshauri wa
watawala, bali, aliwatengeneza watawala ( Kingmaker).
Naam, Mandela anazikwa kijijni kwao
Qunu. Tumeona, kuwa hiki si kijiji alichozaliwa Mandela, alizaliwa
Mvezo. Lakini, huko baba yake Mandela alilazimika kuhama na kwenda Qunu.
Ni baada ya kutoelewana na mtawala.
Katika mazishi ya leo, wengi wamealikwa na Serikali ya Afrika Kusini kwenda kumsindikiza Mandela kwenye safari yake ya mwisho.
Lakini, kuna mtu mmoja ambaye
inasemekana hayumo kwenye orodha ya waalikwa, ni Askofu Desmond Tutu.
Huyu ni rafiki wa miaka mingi wa Nelson Mandela, na si marafiki tu,
wawili hawa, kabla ya Mandela kukamatwa, waliishi nyumba jirani kwenye
kitongoji cha soweto. Ndio, walikuwa majirani wa kuombana chumvi.
Je, ni kwanini jirani wa Mandela wa miaka mingi, Askofu Desmond Tutu, hayumo kwenye orodha ya watakaokwenda kumzika Mandela?
HABARI ZOTE ZIKO HAPA BOFYA HAPA >>HABARI ZETU
No comments:
Post a Comment