Mkurugenzi
wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo
Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa
akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni
majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk
Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu
nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na
kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Wakati
huo huo Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid jana jioni (Jumanne, Novemba 12,
2013), Dkt. Sendongo Mvungi arifariki majira ya saa 8:30 mchana kwa saa
za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
"Kwa
masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt.
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark
iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo
(Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya
Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.
"Taratibu
za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja
nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa leo
(Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.
Marehemu Dkt. Mvungi
alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika
Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake
Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi
vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika
taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia,
ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba
huo.
Picha
juu ikimuonyesha Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam
SULEIMAN KOVA pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani wakionyesha mapanga
yaliotumika kumshambulia Marehemu Dk.Mvungi ni matumaini yetu kwa kuwa
ushaidi umepatikana na baadhi ya watuhumiwa wamepatikana sasa Tunaomba
sheria ichukue mkondo wake kwa unyama huu ili uwe fundisho kwa watu
wengine pia wenye tabia kama hizo.
PUMZIKA KWA AMANI DK.MVUNGI TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
|
No comments:
Post a Comment