Wakati Naibu Spika, Job Ndugai akisema maelezo binafsi ya Mbunge wa Viti
Maalumu, Esther Bulaya (CCM) kuhusu biashara ya dawa za kulevya na
athari zake aliyoyatoa bungeni juzi jioni hayatajadiliwa, Kitengo cha
Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini kimeshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na
wafanyabiashara wa dawa za hizo.
Ndugai alitoa ufafanuzi huo jana baada ya Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi
Lugola kuomba mwongozo jana, akitaka Bunge likubali mjadala wa suala
hilo kutokana na unyeti wake.
Akizungumza na Mwananchi Dar es Salaam jana, Kamanda wa kitengo hicho,
Godfrey Nzowa alisema wameshtukia mbinu mpya zinazotumiwa na
wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao sasa wanatumia barabara badala
ya anga.
No comments:
Post a Comment