Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, August 8, 2013

SERIKALI YA ZANZIBAR YAITISHA KIKAO CHA DHARURA KUJADILI NA KUWASAKA WATUHUMIWA WALIOWAMWAGIA TINDIKALI RAIA WAWILI WA UINGEREZA JANA USIKU MJI MKONGWE ZNZ


 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielezea jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyosikitishwa na Kitendo cha raia wawili wa Uingereza Katie Gee na Kisty Trup cha kumwagiwa tindikali (Acid) na watu wasiojuilikana katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, Kulia yake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed wakiambatana na Bamalozi wa heshima wa Uingereza, Ujerumani an Marekani waliopo hapa Zanzibar.


Kikao hicho cha dharura kilifanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar na kushuhudia pia na baadhi ya Viongozi wa Jumuia za utembezaji watalii za hapa Zanzibar ZATO na ZATI. Picha na Hassan Issa wa – OMPR -- ZNZ.
****************************************

Othman Khamis Ame
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesikitishwa na kitendo kibaya na kiovu walichofanyiwa raia wawili wa kike wa Uingereza Katie Gee na Kisty Trup cha kumwagiwa Tindi kali { Acid } mapema jana usiku katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Raia hao wawili wa Uingereza ambao wamekuja Nchini Tanzania kwa kazi za kujitolea wakiwa hapa Zanzibar kwa matembezi ya wiki wamejeruhiwa katika sehemu zao za uso na vifua na watu ambao mpaka sasa bado hawajajuilikana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Mabalozi wadogo wa Heshima wa Uingereza, Ujerumani na Marekani waliopo hapa Zanzibar walioambatana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo pamoja na Jumuia zinazojihusisha na utembezaji watalii za ZATO NA ZATI.

Balozi Seif alisema kwa kuwa hilo sio tukio la bahati mbaya kufanya hivyo amewaomba wananchi popote pale walipo kujaribu kusaidia kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi mara tuu watakapoona dalili za watu waliohusika na vitendo hivyo.

Alifahamisha kwamba Zanzibar ni moja ya Nchi inayosemwa vizuri katika Nyanja za Kimataifa, lakini kwa mfumo huu uliojichomoza unaofanywa na baadhi ya watu wachache wasioeleweka malengo yao unaweza kukatisha tamaa kwa wale wageni waliojipangia kutaka kutemebelea Zanzibar.

“ Ipo kumbu kumbu hapo nyuma na nyengine si ya muda mrefu ya matukio ya baadhi ya watu kumwagiwa tindi kali { Acid } lakini hichi cha wageni hawa waliokuwa kujitolea hapa Nchini kimewafanya kupewa adhabu wasiyostahiki “. Alielezea Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amewahakikishia Mabalozi hao wadogo wa Heshima hapa Zanzibar wa Uingereza, Ujerumani na Marekani kwamba Serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya ulinzi kwa msaada wa Wananchi itafanya uchunguzi na kuhakikisha wahusika wa kitendo hicho wanatiwa nguvuni ili kupelekwa katika vyombo vya sheria.

Mapema Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema Vijana hao wa kujitolea kutoka Uingereza Katie Gee na Kisty Trup walipatia huduma ya kwanza katika Hoteli ya Tembo iliyopo Forodhani chini ya usimamizi wa Dr. Saleh Mohammed Jidawi Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Alisema tukio hilo la tindikali linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wakorofi kama sialaha kwa kuwaathiri watu wasio na hatia limeleta athari kubwa na kutia doa katika sekta ya Uchumi.

Waziri Mbarouk alimpongeza Balozi wa Heshima wa Uingereza hapa Zanzibar Balozi Carll Salisbury kwa hatua zake za kutoa usafiri wa Ndege ili kusafirishwa kwa vijana hao ili kuendelea kupatiwa matibabu zaidi Mjini Dar es salaam na baadae Nchini mwao.

Wakichangia katika kikao hicho Ofisa wa Ubalozi wa Marekani hapa Zanzibar Jefferson Smith na Balozi wa Heshima wa Uingereza hapa Zanzibar Carll Salisburg walisema Serikali ni vyema ikawa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wakati yanapotokea matukio yasio ya kawaida ndani ya Jamii.

Nao wawakilishi wa jumuiya za watembezaji watalii hapa Zanzibar wameiomba Serikali kutenga fungu maalum kwa ajili ya kuviunga mkono vyombo vya ulinzi katika kukabiliana na matukio yanayoashiria kutaka kuvunja amani na kuhatarisha maisha ya Jamii.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed ameiasa jamii kujenga tabia ya kuchukia jambo lolote baya lionaloonekana kujichomoza miongoni mwao katika maeneo wanayoishi.

Waziri Aboud alieleza kwamba mazingira yaliyopo mitaani hivi sasa yamejidhihirisha wazi kuwa wapo baadhi ya watu wanaoshabikia matendo maovu yanayofanyika katika sehemu zao ambayo wanaelewa wazi kuwa hatma ya matendo hayo hufikia hatua ya kuwaathiri hata wao wenyewe.

No comments:

Post a Comment