Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dakta Shukuru Kawambwa
NI mwezi ujao ambapo itaeleza mchakato mzima wa suala la usahihishaji na upangaji wa mitihani nchini.
Bagamoyo. Serikali
imesema inajiandaa kutoa tamko zito mapema mwezi ujao kuhusiana na
mchakato mzima wa usahihishaji na upangaji wa mitihani ya kidato cha nne
nchini.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameyasema hayo juzi,
alipozungumza na Jumuiya ya Walimu, wazazi na wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Matimbwa wilayani Bagamoyo baada ya kufanya ziara ya kukagua
shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzungumza na wapigakura wa jimbo
lake kuhusu masuala ya elimu na changamoto zilizopo.
Dk
Kawambwa aliwaeleza wananchi jimboni humo kuwa matokeo ya kidato hicho
cha nne mwaka huu, yatapangwa kwa alama za ulinganishi sawa kwa masomo
yote. Waziri huyo aliweka bayana kuwa amekuwa akikerwa na baadhi ya watu
wakiwamo viongozi ngazi za juu kuingiza siasa katika masuala ya elimu
nchini na kuwaomba wananchi kuwapuuza kwani nia yao ni kujipatia
umaaarufu wa maendeleo kupitia suala hio.
Endelea kusoma habri hii kwa kuofya hapa chini
Alisema
kijumla Serikali imekuwa ikikerwa na watu ambao kila kukicha wanaona
njia rahisi ya kujipatia umaarufu ni kutaka kutumbukiza siasa katika
elimu kitu ambacho alisema hakiwezi kukubalika.
“Nimekuwa
nakereka sana na watu wanaotumia matatizo ya walimu, ufaulu wa
wanafunzi na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu, kutaka kujipatia
umaarufu badala ya wao kuchangia mawazo yao ya nini kifanyike ili
kuisaidia Serikali kuboresha hali hiyo”alisema Kawambwa.
Akizungumzia
kuhusu madeni na malimbikizo ya walimu,Kawambwa alisema kwa ujumla
hakuna mtu anayependa kudaiwa hivyo hata Serikali nayo haipendi kudaiwa
inajitahidi kushughulikia ila kinachokwamisha kukamilisha haraka
mchakato huo ni walimu wengi wanaodaiwa kuidai Serikali kushindwa
kuthibitisha madai yao mapema kwa madai wengi wao hawana vithibitisho
vya madai.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment