1. Wema Sepetu
Well, well, well kunaweza kukawa na
mjadala mrefu sana hapa wa kwanini mrembo huyu akamate nafasi ya kwanza
wakati kila kukicha amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa scandals
kibao.
Hiyo ni kweli
lakini ukiugeuza umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa
biashara na jinsi anavyokubalika, hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand
inayouzika kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti ya udaku
ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu
inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa
zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule
unayemjua hapa Tanzania.
Iwe picha akiwa kwa daktari
aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa nywele, tattoo aliyojichora,
picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha zinamuonesha akiwa na shoga
zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu Wema kinavutia attention ya
watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata comments nyingi kuliko za
wengine wote.
Kama leo hii Wema akisema aanzishe
bidhaa yoyote inayowalenga vijana, haitachukua muda kushika na kutafutwa
kama njugu. Wema ni show stopper! Kama akiingia ukumbini kwenye
shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda kutokana na watu kugeuka
kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati akielekea sehemu ya kukaa.
Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa muigizaji wa orodha A Tanzania,
CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame Films, Wema Sepetu ni mwanamke
mwenye ushawishi mkubwa.
2. Diamond
Ni msanii gani Tanzania ambaye nyimbo
zake zinahit mtaani bila hata kupigwa redioni? Bila shaka umeshasikia
nyimbo nyingi za Diamond mtaani siku za hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA
na ukajiuliza iweje unahit wakati haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond
umekuwa ukitumika kama tulizo la wanyonge walio kwenye mahaba mazito.
Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote
zimekuwa zikitumiwa na watu wa rika mbalimbali, madaraja tofauti ya
kiuchumi, wanawake kwa wanaume na watoto kama burudisho la roho zao.
Diamond Platnumz hi hitmaker na haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii anayefanya show
nyingi zaidi ndani na nje ya Tanzania na kwa kulipwa gharama kubwa
kuliko msanii mwingine yeyote muda huu. Hujaza kumbi kubwa za starehe
yeye mwenyewe bila backup ya msanii mwingine na kuwaacha wasichana
wakibubujikwa na machozi ya furaha na kutamani walau kukishika tu kifua
chake kilichoanza kupasuka kwa mazoezi.
Kwa mujibu wa kampuni ya Push Mobile,
Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi
nyimbo zake kama miito ya simu (RBT).
Pamoja na kuzungukwa na scandal kibao
kuhusu wanawake, Diamond ni kijana mwenye mawazo pevu na ya kiutuuzima.
Akiwa ametoka kwenye familia duni na kupata misukosuko mingi ikiwemo
kutengwa na baba yake na kulelewa zaidi na mama yake, Diamond amekuwa
akitoa ushauri na kuwapa moyo watafutaji wa maisha wasikate tamaa.
Hupenda kutoa ushauri kwa vijana wenzie kuhusiana na umuhimu wa
kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu mwenyezi Mungu na kutokata tamaa.
Katika kuhakikisha kuwa anaitolea pia
jamii, hivi karibuni alitangaza kuwa na nia ya kujenga msikiti. Ni kwa
sababu zipi kijana huyu asiwe na ushawishi?
3. Millard Ayo
Japo si kituo chake cha kwanza kuanza
kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha
Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani,
ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika
radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.
Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni
pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na
kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi
ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi
cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM.
Leo hii Millard ni miongoni mwa
watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni
bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi
kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 40,000 kwenye Twitter
huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 90,000.
Umaarufu wake kwenye mitandao ya
kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB
Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu
zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye
wasomaji lukuki. Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea
kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za
mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
4. Nancy Sumari
Nancy Sumari ni msichana mrembo,
mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania wa kwanza aliyewahi kufika mbali
zaidi kwenye shindano la Miss World ambapo mwaka 2005 alifanikiwa kuwa
Miss World Africa.
Kwa sasa Nancy ambaye ni mama wa
mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na anasoma Shahada ya Biashara. Pia ni mjasiriamali na anafanya kazi
zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha watoto wa kike kujitambua na
kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao.
Katika harakati zake za kuhakikisha
wasichana wa Tanzania wanatambua haki zao, anaendesha programu iitwayo
Mentorship, ambayo inazunguka kwenye shule mbalimbali za serikali za
wasichana nchini, na kuzungumza nao kuhusu maisha. “Kwenye programu
hiyo, tunabadilishana mawazo na wanafunzi na wao wanazungumza changamoto
wanazokutana nazo na kupeana mawazo jinsi ya kufanya kwani nawaambia
wakiamua kuthubutu wanaweza kufanikiwa, na wanaonesha wanaweza,”Nancy
aliliambia gazeti la Habari Leo hivi karibuni.
Pamoja na hayo pia Nancy
anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwenye kampeni ya
kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za sekondari za serikali
nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Hivi karibuni alizindua kitabu chake
kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’ kinachomlenga mtoto wa kike kuona jinsi
wanawake wengine walivyofanikiwa licha ya kupitia changamoto mbalimbali.
“Ninaamini kitabu kitasomwa na wengi
ndio maana nikaamua ujumbe wangu niufikishe kwa njia hii, watasoma
watoto wetu hata wajukuu kitajenga kitu kwenye akili ya mtoto na
wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao watathubutu” aliliambia Habari
Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa kutoka kwa mrembo huyu.
5. Ambwene Yesaya aka AY
Safari ya AY mpaka kuja kuwa nyota
anayefahamika Afrika nzima na sehemu zingine duniani haikuwa rahisi.
Amepitia mengi. Aliwahi kusema kuwa kabla ya kufahamika Afrika
Mashariki, alikuwa akienda Kampala na Nairobi kufanya show za bure ili
tu kukuza jina lake, jitihada ambazo zilizaa matunda.
AY ni msanii smart, mbunifu, risk taker na anayeijua biashara ya muziki.
Ni msanii wa Tanzania anayefanya
video za ghali zaidi ambapo mpaka sasa video zake tatu, Speak With Your
Body aliowashirikisha wamarekani Lamyia Good na Romeo, Partyzone na
Money zilimgharimu zaidi ya dola 70,000 kwa pamoja kuzikamilisha. Video
zake zimekuwa zikichezwa kwenye vituo vikubwa vya runinga duniani.
Mwaka jana alifanikiwa kuandika
historia kwa kushinda tuzo za Channel O katika kipengele cha video bora
ya mwaka ya Afrika Mashariki kwa wimbo wake I don’t Wanna Be Alone
aliowashirikisha Sauti Sol wa Kenya. Umaarufu na busara zake ziliivutia
kampuni ya simu ya Airtel mwaka jana na kumteua kuwa balozi wake. Kwa
sasa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya burudani, Unity Entertainment,
anajihusisha na biashara za nguo, mwanzilishi wa kipindi cha
televisheni cha Mkasi na biashara zingine.
Akiwa na followers zaidi ya 40,000
kwenye Twitter, mwaka huu AY amekuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kupata
alama ya tick ya blue ya verification kwenye mtandao huo. Ni watu
watano tu nchini wana alama hiyo.
6. Hasheem Thabeet
Hasheem Thabeet ni mtanzania wa
kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu wa kulipwa nchini
Marekani, NBA. Akiwa na urefu wa 7 ft 3 Hasheem ndiye mchezaji mrefu
zaidi kwenye ligi hiyo. Anacheza timu ya Oklahoma City Thunder kwa
mshahara wa dola milioni 5.128 kwa mwaka.
Pamoja na kuwa Marekani muda mwingi,
Hasheem hasahau ya nyumbani na hupenda sana kuongelea wasanii wa Bongo
Flava kama alivyoandika.
“Mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 Juma
Nature alikuwemo katika kila nyimbo ambayo ilikuwa hit ndani ya bongo.
kubali au kataa. #fact.”
Akitumia Twitter, Hasheem anajulikana
kwa jinsi anavyopenda kuandika ujumbe wa matumaini. Hizi ni tweets 5
zenye ujumbe utiao matumaini alizoandika hivi karibuni.
No matter what u go thru in life
there is no need of gettin angry with god and reflect bitterness to
people around u. #havefaith.
The wise ones speak b’se they have
something to say… fools speaks b’se they have to say somethin. thik
before u speak. #liveandlearn.
Everything can change in a blink of an eye… but dont worry; god never blinks. #believe #havefaith
Life aint about how hard u can hit… it’s about how hard u can get hit and still move forward.
Envy is a waste of time… accept what you already have, not what u need.
7. Flaviana Matata
Flavy ni mwanamitindo wa kimataifa
aliyehamishia makazi yake nchini Marekani. Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
katika fani hiyo kwa kushiriki kwenye fashion show kubwa dunia, kufanya
matangazo ya brand kubwa pamoja na kuhusishwa kwenye majarida ya
kimataifa.
Hivi karibuni Matata alishiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.
Kampeni ya DIESEL + EDUN ilianzishwa
mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL –
Renzo Rosso – na waanzalishi wa kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono
walisafiri hadi nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba
barani Africa.
Waliingia makubaliano ya kutengeneza
nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo
kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama
kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana
mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na
duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss
Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la
Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.
Alianzisha taasisi ya Flaviana Matata
Foundation inayohusika kuwasaidia wasichana kupata karo ya shule, sare
na mahitaji mengine muhimu. Pia hutoa mafunzo na misaada kwa wanawake
ili waanzishe miradi mbalimbali ili kujiongezea kipato.
8. Loveness Diva
Diva Love Loveness ni mtangazaji
maarufu zaidi wa vipindi vya usiku. Ujasiri wake wa kuzungumza masuala
ya mapenzi bila kificho umemtengenezea maisha ya pande mbili, kupendwa
sana na kuchukukiwa sana. Ana mashabiki wengi.
Mara kadhaa kauli zake zimewahi
kuleta mijadala mizito nchini lakini bado kipindi chake cha Ala za Roho
cha Clouds FM kimeendelea kuwa kipindi chenye wasikilizaji wengi zaidi
ukilinganisha na vipindi vingine vya aina hiyo katika vituo mbalimbali
vya radio nchini.
Diva pia hujihusisha na shughuli za kusaidia wasiojiweza kupitia mradi wake wa Diva Giving for Charity.
9. Masanja Mkandamizaji
Huenda watu wengi wanaweza wakawa
hawafahamu kwamba Masanja ndiye staa wa Tanzania mwenye likes nyingi
Facebook, 104,670 na zaidi. Masanja ni miongoni mwa wachekeshaji wa
kizazi kipya wenye mashabiki wengi zaidi. Umaarufu wake umetokana na
kipindi cha Ze Komedi kilichoanzisha EATV na sasa kikiwa TBC 1. Pamoja
na kuwa mchekeshaji, Masanja ni muimbaji wa nyimbo za injili, mchungaji
mtarajiwa na mambo mengine. Huzitumia akaunti zake za mitandao ya
kijamii kuchekesha na kuwafurahisha zaidi followers wake na ni miongini
mwa mastaa wanaopata comments nyingi zaidi kila wawekapo status.
Hamis Corlone Mwinjuma aka Mwana FA
ni rapper anayeaminika kuwa miongoni mwa waandishi bora wa mashairi ya
Hip Hop kuwahi kutokea katika muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Jina lake lilianza kuvuma mwaka 1998
alipotoa ngoma yake ‘Ingekuwa Vipi?’ akiwa na Jay Mo na pia ‘Mabinti’
ambayo ilitayarishwa na Bonny Luv.
Mwaka 2003, ngoma yake ‘Alikufa Kwa
Ngoma’ – ilimpa tuzo kama wimbo bora wa Hip Hop wa mwaka kwenye Kili
Music Awards. Mwana FA aliendeleza utemi kwa kuachia hits kibao kama
Unanitega, ‘Hawajui’ feat. Lady Jaydee, Habari Ndio Hiyo akiwa AY, Bado
Nipo Nipo, Unajijua Unanisikia, Yalaiti na ngoma ya hivi karibuni Ameen.
Mwaka huu anasubiriwa kwa hamu kuachia ngoma yake mpya iitwayo Kama Zamani aliyowashirikisha Njenje.
Pamoja na kufanya muziki, Mwana FA
aliamua kwenda nchini Uingereza kuongeza shule yake ambako alisoma
shahada ya Finance katika chuo kikuu cha Coventry.
Ana mipango pia ya kuendelea na
masomo ya PhD siku za usoni. Kwa sasa ameanzisha pia kampuni ya
kusimamia wasanii iitwayo Lifeline Music Inc ambayo tayari ina msanii
mmoja aitwaye Maua Sama.
11. Salama Jabir
Salama ni mhasisi wa kipindi cha
Planet Bongo cha EATV ambacho enzi anakifanya kilichangia ubora wa video
za muziki wa Bongo Flava nchini kutokana na kasumba yake ya kuzikosoa
bila woga. Baada ya kuondoka EATV na East Africa Radio, Salama alienda
kusoma nchini Uingereza na kurudi kukaa nje kwa muda na mambo ya habari.
Alikuja kurejea tena na kipindi cha Mkasi kinachorushwa EATV na
kukifanya kuwa kipindi bora kabisa cha mahojiano nchini. Salama ni
mcheshi, mtundu na anaufahamu mkubwa wa masuala ya burudani. Namna ya
uulizaji wake wa maswali hufanya vipindi vyake kuwa na mvuto zaidi.
12. Fid Q
Fareed Kubanda si rapper
anayeheshimika tu kama mwandishi mkali wa mashairi, bali pia
anatambulika kwa kujihusisha kwake na shughuli za kijamii.
January mwaka huu, Taasisi ya Under
The Same Sun inayojihusisha na kutetea haki ya watu wenye ulemavu wa
ngozi, albino nchini, ilimtunuku ‘cheti cha shukrani’ kwa mchango wake
katika kampeni ya shirika hilo.
Alipata cheti hicho baada ya mwaka
jana kujumuika na taasisi hiyo katika ziara yao ya kanda ya ziwa akiwa
kama muelimishaji kwenye vita dhidi ya mauaji ya ALBINO.
“Kujituma kwenye uchapaji kazi na
utaratibu wa kuwa na nidhamu kazini ni moja kati ya vitu
vilivyowafurahisha,” aliiambia Bongo5.
Pia mwaka jana Fid alikuwa akiendesha darasa la hip hop la hiari jijini Dar es Salaam.
Akielezea madhumuni yake, Fid
alisema, “Kwa haraka haraka hip hop darasa maudhui yake ni kuwafundisha
vijana wawe na positive thinking na attitude kwa jamii, yaani wawe na
fikira zilizopo katika mstari ulio sahihi na hata kitabia, kwahiyo
tunawajenga hivyo kupitia muziki wa hiphop.”
13. Lady Jaydee
Mpaka sasa Lady Jaydee ana albam tano
na hivi mwezi ujao ataachia albam ya sita aliyoipa jina NOTHING BUT THE
TRUTH. Ndiye msanii wa kike Tanzania anayeheshimika na mwenye mafanikio
zaidi. Jaydee ni mjasiriamali ambaye hutumia pia kipato anachokipata
kwenye biashara zake kusaidia watu wanaohitaji msaada hususan watoto
yatima wanaolelewa kwenye vituo maalum.
Mwaka huu Lady Jaydee ambaye ana
likes zaidi ya 47,000 Facebook na followers zaidi ya 22,000 Twitter,
aliweka historia kwa kufanikisha safari ya kuupanda mlima Kilimanjaro na
kuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kufanya hivyo.
13. Jacob Stephen
Jacob maarufu kama JB, ni muigizaji
ambaye wachambuzi wa filamu za Tanzania wanadai kuwa msanii pekee wa
kiume anayeweza kufikia mafanikio ya marehemu Steven Kanumba. Ni
muigizaji wa kiume anayependwa zaidi kwa sasa na filamu zake zimekuwa
kivutio kwa watu wengi wa kila rika. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 14
kwenye sanaa ya uigizaji.
Kwa sasa anamiliki kampuni ya filamu
iitwayo Jerusalem ambayo imesaidia kuwaibua wasanii wengine akiwemo Rose
Ndauka, Elizabeth Kiyumba ’Nikita’ na wengine.Pamoja na kuwa muigizaji
pia JB ni mhubiri wa masuala ya dini.
15. Jokate Mwegelo
Jokate ni mtangazaji wa TV (Channel
0), muigizaji wa filamu, mwanamuziki na mjasiriamali. Umaarufu wake
ulianza aliposhiriki shidano la Miss Tanzania mwaka 2006 na kukamata
nafasi ya pili na kupata ubalozi wa Redd’s na gazeti la The Citizen.
Jokate amewahi pia kushinda tuzo za
ZIFF kama muigizaji bora wa kike. Pamoja na hivyo hujihusisha na muziki
pia ambapo amewahi kushirikishwa na AY kwenye wimbo Kings and Queens na
hivi karibuni amesikika kwenye wimbo wa Lucci, Water up.
Hivi karibuni alijiingiza kwenye
biashara ya ubunifu wa mitindo kwa kuanzisha kampuni na brand ya Kidoti
ambayo hubuni nguo pamoja na kutengeneza nywele za aina mbambali
zinazopatikana nchini.
16. Vanessa Mdee
Vanessa ni mtangazaji mahiri wa MTV
Base na Choice FM. Uwezo wake mkubwa wa kutangaza, maarifa kuhusu
burudani na mambo mengine vimemfanya awe miongoni mwa watangazaji wa
kike wakali zaidi barani Afrika na wenye mashabiki lukuki.
Vanessa amefanikiwa pia kwenye muziki
ambapoi alimake headline sana aliposhirikishwa na Ommy Dimpoz kwenye Me
and You iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana. Sauti tamu kwenye chorus
hiyo iliwashtua wengi kwakuwa alikuwa akijulikana kama mtangazaji tu.
January mwaka huu aliachia single
yake ya kwanza Closer. Ngoma hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki wa
muziki na miongoni mwa nyimbo zilizopata downloads nyingi zaidi
mtandaoni. Na sasa ametajwa kuwania tuzo za Kili kama msanii bora
anayechipukia huku wimbo Me and You alioshirikishwa na Ommy ukitajwa pia
kwenye vipengele kibao. Ashafanikiwa kushare stage moja na wasanii wa
kimataifa wakiwemo Mi Casa Music wa Afrika Kusini.
17. Rita Paulsen
Maadam Rita anafahamika zaidi
Facebook kwa wafuasi wake zaidi ya 25,000 kama mwanamke mwenye ushauri
muhimu kuhusu maisha. Ni mwanzilishi wa shindano kubwa la kusaka vipaji
vya kuimba nchini, Bongo Star Search ambalo limefanikiwa kutoa vipaji
vingi na kwa kuwazawadia washindi vitita vya pesa. Ni mcheshi, mrembo na
ambaye siku zote hupenda kuwapa moyo hata wale ambao uwezo wao ni
mdogo.
18. Profesa Jay
Profesa Jay ni miongoni mwa wasanii
waliyoifanya Bongo Flava ipate mafanikio. Akiwa na albam nne mpaka sasa,
Machozi Jasho na Damu 2001, Mapinduzi Halisi 2003, J.O.S.E.P.H 2006 na
Aluta Continua 2007, Prof amewahi kushinda zaidi ya tuzo 6 mbalimbali
zikiwemo za Kili. Mpaka sasa hits zake zikiwemo Bongo Dar es Salaam,
Jina Langu, Zali la Mentali, Nikusaidije na zingine zinaendelea kutoa
burudani isiyo na kifani katika masikio ya mashabiki wake.
19. Fetty
Fetty aka Fetilicious ni Dj pekee wa
kike wa Tanzania aliyefanikiwa hadi mwaka jana kupata shavu la kwenda
kupiga muziki kwenye jumba la Big Brother Africa. Ni msichana mrembo,
anayejiamini na machachari hewani huku akiwa na fanbase ya nguvu. Ana
likes zaidi ya 57,000 kwenye Facebook na followers zaidi ya 25,000
kwenye Twitter. Pamoja na kuwa mtangazaji wa kipindi pendwa cha XXL,
Clouds FM, Fetty ni dj kwenye club ya Ambassodors Lounge jijini Dar.
20. Mzee Majuto
Kwa wengi King Majuto ni mchekeshaji
bora zaidi nchini kuliko wachekeshaji wote. Ni comedian wa kuzaliwa
ambaye sura yake tu huwavunja mbavu watu. Filamu zake zinauzika zaidi
huku akiwa na mashabiki kibao katika nchi zingine za Afrika
zinazozungumza Kiswahili. Umaarufu wake umemfanya apate deals za kufanya
matangazo mbalimbali yakiwemo ya Airtel na Azam.
“Jina la King Majuto limeweza kuwa
maarufu zaidi kwake, kutokana na kazi yake ya uigizaji katika filamu za
vichekesho, mafanikio yake katika uigizaji yamefanya waigizaji chipukizi
kutamani kumshirikisha msanii huyo mkongwe na wengine kujifunza kupitia
kwake. Wapo wasanii chipukizi ambao wanatamani kufika kiwango
alichofikia King Majuto, akitamba katika fani kwa zaidi ya miongo mitatu
sasa bila kuchuja wala kutetereka
No comments:
Post a Comment