Na Fredy Azzah na Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam. Maswali juu ya utaratibu
uliotumika kutoa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye Akaunti ya Escrow
katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina ya Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL yameanza kupata majibu.
Wakati mmiliki kwa Kampuni ya VIP Engineering and
Marketing, James Rugemalira ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni mwa
waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa IPTL ukifafanua utata kuhusu
mkataba wake na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa jumla kwa Pan
African Energy.
Majibu ya Rugemalira
Katika ufafanuzi wake, Rugemalira alisema kati ya
fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow, yeye akiwa mwanahisa wa IPTL
alilipwa Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni), alizoziita
‘vijipesa vya ugoro’ sawa na asilimia 30.
Alisema baada ya kuuza hisa zake kwa Kampuni ya
Pan African Power (PAP) aliruhusu pia asilimia 70 ya hisa za mbia
mwenzake, Mechmar kutoka Malaysia ziuzwe pia kwa PAP.
Alisema kwenye akaunti hiyo kulikuwapo na Dola za
Marekani 120 milioni, tofauti na kiwango kilichotajwa na Gavana wa BoT,
Profesa Benno Ndulu aliyesema fedha hizo zilikuwa Dola 122 milioni.
Rugemalira alisema pia kuwa hatua ya kufikiwa kwa
hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji John
Utamwa Januari 17, mwaka 2014 saa 8: 30 usiku, ilitokana na Waziri wa
Nishati kumuomba wamalize kesi zilizokuwa mahakamani.
“Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi
tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means’ (jambo la
muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa
masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo
vijipesa vya ugoro,” alisema Rugemalira.
Hatua ya kutoa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya
Escrow na kugawiwa kwa VIP Engineering na PAP, imefikiwa huku mkopeshaji
wa IPTL, Benki ya Standard Charted ya Hong Kong (SCB-HK), inayodai Dola
za Marekani 145 milioni (Sh234.456 bilioni), ikiwa haijalipwa na wala
haijajulikana italipwa kwa kutumia kanuni gani.
Itakumbukwa kuwa, baada ya benki za Malaysia
zilizokuwa zimeikopesha IPTL kuyumba kiuchumi, deni la benki hizo
lilinunuliwa na SCB-HK.
“Tumeridhia kuwa hizo asilimia 70 zichukuliwe na
PAP na Standard Charted anadai kwamba yeye ndiye mkopeshaji na dhamana
yake ni hiyo mitambo, kitu ambacho siyo kweli. Lakini kama ni kweli
aende mahakamani kuthibitisha,” alisema Rugemalira.
Hukumu iliyotolewa Februari 12, 2014 na Kituo cha
Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Washington DC,
Marekani, ilitaka pande hizo mbili zikae na kukubaliana namna ya
kukokotoa gharama
No comments:
Post a Comment