
Dawa ya kulevya aina ya Heroine na bomba la sindano
Polisi nchini Tanzania
wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo
201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar nchini
humo.
Kamanda wa kikosi maalum cha kuzuia dawa za
kulevya Godfrey Nzowa ameiambia BBC kuwa Watu 12 wanashikiliwa kuhusiana
na shehena hiyo .
Kamanda Nzowa amesema dawa hizo za kulevya
zimekamatwa na Polisi wa doria baharini muda wa saa sita usiku wa
kuamkia Jumanne zikisafirishwa katika Jahazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Shehena hiyo ilikuwa
ikitoka nchini Iran kuelekea nchi au eneo ambalo mpaka sasa bado
halijafahamika.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kukamata
dawa za kulevya aina mbalimbali kupitia viwanja vya ndege,nchi kavu na
baharini, ambapo mwaka jana kiasi kikubwa cha dawa za kulevya
zilizokamatwa ziliteketezwa
No comments:
Post a Comment