Makala: Sifael Paul na Mitandao
NI jabali wa Afrika. Baba wa Taifa la
Afrika Kusini. Alikuwa kipenzi cha wengi, Nelson Rolihlahla Madiba
Mandela ‘Mzee Madiba’ (95). Alifariki dunia Desemba 5, mwaka huu na
kuzikwa jana kijijini kwake, Qunu huko Eastern Cape, Afrika Kusini.
Huwezi
kuacha kumzungumzia. Ana vitu vingi hasa juu ya maisha yake. Makala hii
inalenga kuangalia maisha yake ya kifamilia hasa kipengele cha mapenzi.
Kubwa ni mapenzi yake na mkewe wa tatu, Graca Machel ambayo yanaelezwa
kuwa kama ya njiwa.
Tunajua
katika maisha kuna wakati mtu unakutana na vipingamizi vya kufikia
malengo kutoka ndani ya familia au jamii inayokuzunguka.
Baba yake alifariki dunia wakati Mzee
Madiba akiwa na umri wa miaka tisa tu kwa hiyo hakuna mchango wa mzazi
huyo kwenye harakati zake za kutetea haki za mtu mweusi.
Alipoanza
mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote,
ilitegemewa kuwa mkewe ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
mafanikio yanapatikana.
Mzee Madiba alioa mara tatu. Mke wa mwisho alimuoa alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa.
Mzee
Madiba katika kipindi chote cha historia ya maisha yake amekuwa mtetezi
wa watoto kupitia Mfuko wa Nelson Mandela wa kusaidia watoto.
Mzee Madiba ni baba wa watoto sita.
Wanne aliwazaa na mkewe wa kwanza, Evelyn Mase na wawili alizaa na mke
wake wa pili, Winnie Madikizela Mandela.
Baadhi ya watoto wake hawakwenda kumuona wakati akiwa gerezani.
Maajabu! Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie!
Mtoto wake wa kwanza alifariki dunia
akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la
Madiba Thembikile (Thembi) alifariki dunia katika ajali ya gari mwaka
1969 akiwa na umri wa miaka 25.
Mwanaye Makgatho alifariki dunia kwa
Ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2005. Watu walipotaka kuficha kilichomuua, Mzee
Madiba aliingilia kati na kusema hadharani kuwa Ukimwi ndiyo umemuua!
Kuanzia hapo Mzee Madiba amekuwa mstari wa mbele kupiga vita Virusi vya
HIV na Ukimwi akitumia namba 46664 ambayo ni namba aliyopewa alipokuwa
gerezani.
Mzee Madiba na Evelyn (yule mke wa kwanza) walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla ya kuvunjika mwaka 1957.
Evelyn alikuwa muumini wa Dhehebu la
Mashahidi wa Yehova ambalo lilikuwa haliruhusu waumini wake kushiriki
kwenye siasa, akashindwa kumsapoti mumewe, Alifariki dunia mwaka 2004.
Mwaka
mmoja baadaye, 1958 Mzee Madiba alimuoa Winnie Madikizela. Winnie
Madikizela Mandela alizaliwa Sauzi Septemba 26, 1936. Ni mwanasiasa
aliyewahi kushika nafasi kadhaa serikalini na kwenye chama kama vile
African National Congress Women’s League.
Kwa
sasa ni mwanachama katika Chama cha National Executive Committee.
Japokuwa aliolewa na Mzee Madiba, wakati mzee huyo anapata urais hakuwa
‘first lady’ kwani wawili hao walikuwa wameshaachana kwa madai kuwa
Winnie, alikuwa siyo mwaminifu baada ya Mzee Madiba kutoka gerezani
ambapo alimpa talaka rasmi Machi 19,1996.
Pamoja
na kuwa mpigania haki maarufu kwa wanachama wake ambao humwita ‘Mama wa
Taifa’ lakini alishindwa kuzuia tamaa ya mwili na kujikuta akimsaliti
Mzee Madiba.
Muda
mwingi hawakuishi pamoja kwa sababu Mzee Madiba alikuwa akitumikia
kifungo huku Winnie akijijengea umaarufu katika majukwaa ya siasa.
Mwaka
1998, Mzee Madiba alimuoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa
Rais wa Msumbiji, Hayati Samora Machel. Wameishi wote katika siku zao za
uzeeni huku wakipeana sapoti ya hali ya juu lakini hawakujaliwa mtoto.
Wawili
hao walipendana mno. Mara nyingi walipoonekana kwenye alaiki walikuwa
wameshikana mikono na kuoneshana mapenzi. Mabusu ya kiutu uzima
yalitawala. Itabaki kuwa ‘pea’ bora zaidi hapa duniani.
No comments:
Post a Comment