Mapenzi na kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao hasa
kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na
kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa
kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu.
Siri ya kufurahia tendo la ndoa ni
wanandoa wote kuridhika na utendaji wa mwenza wao hasa wakati wa tukio,
kwa kujituma, kuwa mbunifu, kutaka na kufurahia tendo hilo. Ingawa ni
kweli kwa nadra inaweza tokea mwenzako akawa na hamu na wewe usiwe nayo
(ikitokea mara chache sana – hili linaeleweka, na linaweza kukubalika
ila si kwa kuzoea na ikawa utamaduni; iwe kwa mwanaume ama mwanamke) .
Izingatiwe kuwa, kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi rahisi…
Mazingira ya kufurahia tendo hili muhimu ni lazima yajengwe na
yaimarishwe mara kwa mara. Maana ni wazi kuwa uhai wa kila ambalo
linatakiwa kuishi ni lazima litunzwe kwa umakini na kujali. Hivyo
kufurahia tendo la ndoa pia hupaswa kuimarishwa kwa nilivyotaja hapo
awali – Kupenda, kujituma, utundu, maarifa na Ubunifu. Na haya yote huwa
rahisi sana ikiwa mwanandoa wako wampenda ama kumkubali, na kubwa
kuliko ikiwa na yeye pia hujituma, ‘ni mtundu’ na ana maarifa pia.
Hivi vitu (Kujituma, utundu, maarifa na ubunifu) haviji hivi hivi pia…
Na ndio kwa misingi hiyo wanandoa hushauriwa kuzungumzia tendo la ndoa,
kama haridhiki katika tendo, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda,
wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho
kinakupandisha mzuka – huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha
unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata
raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo (TAHADHARI – Yapaswa kuwa na
mipaka pia).
Mnaweza msiwe kila mmoja si mtaalam kwa mwenzie mnapoanza
mahusiano yenu ya mapenzi, ila inapaswa na ni jukumu la kila mmoja
kuhakikisha ufundi huo unaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kwa
mwenza wake huyo na si kupungua. Izingatiwe pia kuwa, Kufanya mapenzi si
lazima ukafanya kama vile ambavyo picha za ngono huonyesha ili kujua
mnafurahia, msingi ni kutafuta rhyme ambayo huwafanya wote mfurahie tendo hilo la ndoa na kuwafanya kuwa na kiu juu ya mwenza wako pale unapokuwa umemkosa.
Ndoa si kufanya tu Mapenzi ni zaidi ya hapo,
ila mwisho wa siku kufanya Mapenzi ni muhimu mno kwa ustawi wa ndoa
kati ya wanandoa. Ni suala ambalo kiharaka haraka linaweza chukuliwa kwa
wepesi, ila mwisho wa siku lina faida sana.
FAIDA YA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA
Linajenga ukaribu zaidi kwa wanandoa
Tokana na majukumu ya kifamilia
ambayo yanaenda yakikua kwa kasi na kufanya baadhi ya wanandoa kutokuwa
na wakati wa kuwa karibu zaidi kunakuwa na muda mchache kwa baadhi
kubadilishana mawazo. Wanandoa wengine wamefaulu kwa kuhakikisha kila
siku/au mara kadhaa kwa juma kujulishana habari zao wanapokuwa hawapo
pamoja. Tendo la ndoa linaweza tumika kama wakati muafaka wa kila mmoja
kutiririka na kuongea mambo mbalimbali na hata kupanga mipango yenu ya
kimaisha. Hilo hutokea pale mnapokuwa mnataka kujianda, nusu fainali au
baada ya mchezo kuisha tegemeana na mtiririko wenu upo vipi.
Kumwelewa Mwenzi wako
Tendo la ndoa lina lugha yake… Tendo
hili haliishi tu katika kufurahia na kufika kileleni bali pia linasaidia
kumwelewa na kumsoma mwenzi wako. Ndio maana ni vema sana kumjulia
mwenza wako kitabia na mwenendo kwa kuhusisha tendo hilo. Ikiwa wenza
mna tabia ya kushirikiana na kuhusishana katika masuala ya kila siku ni
rahisi kutambua kuwa mwenza wako siku hiyo kachoka, kachukizwa (iwe na
wewe ama mtu mwingine), ana mawazo, ana wasiwasi, hana raha n.k.
Haijalishi kuwa mwenza wako yupo
katika hali ipi wengi hujitahidi hilo lisiwe kikwazo kwa tendo la ndoa
(hasa wanaume) – Hivyo ni rahisi kumjulia tokana na namna mnavyokuwa
faragha kujua kuna jambo ama la. Ni wazi wakati mwingine kunaweza kuwa
na jambo na mwenzi wako asikuhusishe, kupitia tendo la ndoa unaweza pata
viashiria.
Inasaidia wanandoa kupata Watoto
Watoto wana raha yake katika ndoa, na
wana nafasi kubwa sana katika kuweza kuimarisha ndoa, kuleta furaha
katika familia, kuwajenga na kuwa komaza kama wazazi na pia
kuwaunganisha zaidi wanandoa kama mwili mmoja. Si wote wamejaaliwa
kupata watoto (my heart goes out to them) – ila ukweli ni kuwa mara
nyingi hiki ni kipengele muhimu katika ndoa ambacho wanandoa wenyewe na
jamii hutarajia kuwa muhimu kufanikisha ili ndoa ionekane kuwa ina
mafanikio. Niongeze kuwa tumepishana kutafsiri mafanikio ni nini katika
ndoa, ila wengi huwa na msimamo wa kuwa watoto ni muhimu katika ndoa.
Kutatua ugomvi/mgogoro kati ya wenza
Ugomvi haukwepeki hata kama mwapendana vipi (ingawa frequency ya
ugomvi hupishana kati ya wanandoa). Tendo la ndoa linazungumza mambo
mengi sana…. Kitendo cha kukutana kimwili na mwenza wako kwa namna moja
wapo inakuwa ni akili na mwili wako kukubali kuwa umejitoa kwa mwenzi
wako kwa wakati huo. Kuna makabila ambayo hata uwe umegombana vipi na
mke/mume wako, ikitokea tu ukalala naye na kufanya tendo la ndoa
haijalishi kosa lilikuwa ni lipi inachukuliwa limesamehewa na yapaswa
kusahau na kusonga mbele.
Kupunguza uchovu/Msongo wa mawazo
Ndoa ni moja ya njia kwa baadhi
kuweza kupunguza uchovu alio nao na kwa wengine hata msongo wa mawazo.
Tendo likifanywa vema na kwa ustadi, huweza kumwondolea mwenzi wako
uchovu au msongo wa mawazo kwa kiwango kikubwa. Unafuu huo utegemea
lakini, wengine inakuwa tu unafuu wakati wa tendo hilo na hali wengine
hupata nafuu ya muda mrefu. Hivyo ikiwa mwenzi wako yupo katika hali
hiyo katika kutafuta namna ya kuhakikisha anapata unafuu, unaweza tumia
tendo la ndoa kama silaha ya kumrudisha mwenzi wako katika hali nzuri.
Linajenga heshima ndani ya ndoa (hasa kwa wanaume)
Hili linawezekana pande zote (mke na
mume) mmelipa umuhimu wa pekee tendo la ndoa hadi mkiwa faragha wote
hufurahia tendo hili hadi kuna wakati mwajihisi mpo mwili mmoja kama si
ndani ya ngozi moja. Tunarudi palepale, kuwa ni muhimu ukampenda mtu
wako, ukapenda hilo tendo, mengine yanafuata mkiwa faraghani.
Linatumika kupata unachotaka/Kulaghai (hasa kwa wanawake)
Hili linategemea unalifanya kwa namna
ipi… Ukilifanya kana kwamba ni hongo ya lazima na kuwa wamaanisha
hutokubali kuwa faragha bila kutimiziwa kitu Fulani – Hapo inakuwa ni
tatizo na ndio ulaghai wenyewe. Ila lifanywapo kwa upendo, utani wa
kimapenzi, kwa kutoa maneno matamu na kubembembeleza, husaidia kuongeza
ashiki kwa wapenzi (inaweza isiwe kwa wote) na huku pia ukifanikiwa
kupata kile ambacho unataka mwenzio akiwa katika mood nzuri.
No comments:
Post a Comment