UKIMWI
(HIV) ikiwa bado ni janga la dunia, vile vile Kifua Kikuu (TB) ni
tishio la afya ya jamii kwa kuwa huathiri moja ya tatu ya idadi ya watu
duniani na bado Kifua
kikuu (TB) ndio
ugonjwa unaoua zaidi kwa watu wenye Virusi vya UKIMWI/VVU (HIV) ingawa
kuna chanjo ya utotoni ya inayotolewa kukinga Kifua kikuu (TB). Kila
mwaka Kifua kikuu (TB) huua watu milioni 2 duniani kote.
Chanjo mpya ya Kifua kikuu (TB)
imegunduliwa na Chuo Kikuu cha McMaster inaleta matumaini mapya duniani
kupambana na Kifua kikuu (TB).
Dkt. Fiona Smaill, Profesa na Mkuu wa
kitengo cha Patholojia na Tiba za Molekyuli wa Shule ya tiba ya Michael
G. DeGroote katika Chuo kikuu cha McMaster alisema, 'Sisi ni wa kwanza
kutengeneza chanjo ya aina hii kwa ajili ya Kifua kikuu (TB)'.
'Mapambano dhidi ya Kifua kikuu (TB)
yamekutana na changamoto ya kiwango cha juu cha Kifua Kikuu sugu
(Multi-Drug Resistant Tuberculosis) kisichotibika kwa dawa za kawaida.'
Dkt. Fiona Smaill aliongezea. Hali hii inadhohofisha kampeni ya dunia
dhidi ya Kifua kikuu (TB) yenye lengo la kupunguza maambukizo hadi nusu
kufikia 2015.
Chanjo mpya iliyogunduliwa itaongeza
nguvu kwa chanjo ya Bacille Calmete Guerin (BCG) ambayo hutolewa utotoni
na ambayo ni chanjo pekee ya Kifua kikuu iliyopo.
Chanjo ya BCG imegunduliwa miaka ya
1920 na inatumika dunia nzima. Kwa sasa chanjo ya BCG ni sehemu ya
programu ya chanjo ya Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) katika Asia,
Afrika, Ulaya Mashariki na Amerika ya Kusini, pamoja Nunavat eneo pekee
la ambapo chanjo ya BCG hutolewa. Chanjo hii hutolewa mwaka wa kwanza wa
uhai.
Chanjo mpya imetegemea sana virusi
baridi waliotengenezwa kijenetiki. Chanjo imeandaliwa katika maabara ya
Zhou Xing, Profesa wa Patholojia na tiba za molekyuli katika kituo cha
utafiti wa kinga za mwili cha Chuo kikuu cha McMaster.
Chanjo ya McMaster imekuwa
ikitengenezwa kwa zaidi ya muongo mmoja. Watafiti wa McMaster walianza
majaribio ya kwanza kwa binadamu 2009, kwa watu 24 waliojitolea wenye
afya njema, ikijumuisha watu 12 ambao mwanzo walipata chanjo ya BCG.
Kufikia 2012 walithibitisha chanjo
hiyo kuwa salama na ilifanya mfumo wa kinga mzuri dhidi ya Kifua kikuu
(TB) kwa washiriki 12. Hata hivyo Xing alisema inahitaji majaribio zaidi
kuleta mafanikio zaidi.
Kifua kikuu (TB) ni ugonjwa
unaoambukizwa kwa njia ya hewa, ukisababishwa na bakteria waitwao
Mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu (TB) huanza kuathiri kwanza
mapafu, ila inaweza athiri viungo vingine ndani ya mfumo wa fahamu,
mfumo wa kinga, mfumo wa damu n.k
Mtu anapoambukizwa na kifua kikuu
(TB) bakteria huingia kwenye mapafu na kuzaliana na husababisha Homa ya
mapafu (Pneumonia) ikiambatana na maumivu ya kifua, kukohoa damu na
kukohoa mfululizo kwa zaidi ya ya wiki 2.
Dalili zingine ni kupungua uzito,
kuchoka mwili wote, kutoka jasho usiku na kukosa hamu ya kula, kuumwa na
kifua hasa wakati wa kupumua.
Kama mfumo wa kinga za mwili ukishindwa kupambana na bakteria ugonjwa huzidi na kuharibu mifupa, figo, uti wa mgongo na ubongo.
Ingawa kila mtu anaweza kuambukizwa ila makundi yafuatayo yapo katika hatari zaidi ya kuambukizwa Kifua kikuu (TB) :-
- Wagonjwa wa UKIMWI (HIV), kisukari & kansa/saratani.
- Watu wanaoishi na wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) ambayo haijatibiwa.
- Watu maskini au wasio na makazi maalumu.
- Wazee na wafungwa.
- Walevi na watumiaji wa madawa ya kulevya ya kujidunga.
- Watu wanaotaabika na utapiamlo.
- Watumishi wa afya.
- Wafanyakazi wa kambi za wakimbizi.
- Watu wanaoishi na wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) ambayo haijatibiwa.
- Watu maskini au wasio na makazi maalumu.
- Wazee na wafungwa.
- Walevi na watumiaji wa madawa ya kulevya ya kujidunga.
- Watu wanaotaabika na utapiamlo.
- Watumishi wa afya.
- Wafanyakazi wa kambi za wakimbizi.
Kifua kikuu (TB) hugunduliwa kwa
kuchukua kipande cha ngozi na kukifanyia uchunguzi (Mantoux test),
kupima makohozi, kupiga picha za X-ray & Computer Tomography (CT)
Scan.
Kifua kikuu (TB) hutibika na matibabu
yake hutegemea hali ya mgonjwa. Jambo linalofariji zaidi ni kwamba
nchini mwetu uchunguzi kujua kama umeambikizwa Kifua kikuu (TB) na
matibabu yake ni bure kabisa katika vituo vyote vya afya vya serikali
pamoja na hospitali.
Njia bora ya kudhibiti Kifua kikuu
(TB) hujumuisha kula mlo kamili unaosaidia kuweka vizuri mfumo wa kinga
mwilini, kupima Kifua kikuu (TB) kama upo katika mazingira hatarishi na
pia kusaidia wagonjwa wa Kifua kikuu (TB) kukamilisha matibabu yao.
No comments:
Post a Comment