MTU mmoja mkazi wa eneo la Sakina jijini Arusha aliyefahamika kwa jina
la JAPHET MINJA amemwagiwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni tindikali usoni
na mkononi na watu wasiojulikana katika eneo la Shamsi kata ya Elerai na
kumsababishia majereha.Akizungumza katika hospitali ya Selian
alikolazwa kwa matibabu MINJA ambaye ni fundi ujenzi amesema ametokewa
na tukio hilo jana majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la shamsi
Drive in wakati akitoka nyumbaji kwake akiwa ndani ya gari ambapo
alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya kufanya
biashara na ghafla wakiwa njiani walimgeuka.Daktari wa zamu
aliyempokea mgonjwa huyo GODBLESS MASAWE amesema walimpokea jana asubuhi
akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na kulazimika kumpeleka
katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwa kwa sasa hali yake
inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia kwa kamanda
msaidizi ASP JAPTET LUSINGI amesema bado hawana taarifa kuhusiana na
tukio hilo.
No comments:
Post a Comment