Wawekezaji
wakubwa watatu wa kampuni ya Microsoft ya Marekani wamemshinikiza
mwenyekiti wa kampuni hiyo Bill Gates aachie ngazi ya uenyekiti baada ya
kukalia kiti hicho kwa miaka 40 toka ilipoanzishwa.
Kwa
mujibu wa Skynews ripoti zinasema kuwa wawekezaji hao wanadai kuwa
uwepo wa Mr Gates katika bodi ya wakurugenzi inazuia mabadiliko ya mbinu
mpya za maendeleo ya kampuni hiyo na kuweka ugumu kwa Chief executive
wa sasa kufanya mabadiliko makubwa.
Taarifa
hii imekuja siku chache toka CEO wa Microsoft Steve Ballmer kutangaza
kujiuzulu ndani ya mwaka mmoja kufuatia shinikizo kutoka kwa waungaji
mkono, wakati kampuni inajipanga upya na mapambano ya ushindani mkubwa
katika sekta ya teknolojia.
Hata
hivyo Microsoft bado ni moja kati ya makampuni ya teknolojia yenye
thamani duniani, na hisa zake zimeendelea kubaki na thamani kwa
takribani miaka 10 kutokana na nguvu ya Ballmer ya kupambana na Apple na
Google.
Bill
Gates alikuwa Chief Executive Officer wa Microsoft mpaka mwaka 2000
alipomuachia Ballmer nafasi hiyo na yeye kubaki kuwa mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment