Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’.
MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameswekwa rumande kwa kudaiwa kuchoma nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez Mabovu’, Mashaka Mrisho.
Tukio
hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo mwenye nyumba sambamba na
polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa madai ya kuchoma moto
nyumba kwa makusudi na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
“Mkewe
alitupia mkaa wa moto katika sofa, likashika moto kabla majirani
hawajanisaidia kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha
ndipo nikawapeleka polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja
kumkamata,” alisema Mashaka.
Dudu
Baya alipotafutwa na mapaparazi wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa sero
kwa saa sita kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake aliyemtaja kwa
jina la Vero.
“Vyumba
vyake na vyangu haviingiliani kabisa, tumetenganishwa na ukuta hivyo
shutuma zake hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi wa polisi
ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu baya.
No comments:
Post a Comment