Gari
la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick likiwasili Dampo kuu
la taka la Pugu Kinyamwezi, lililopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini
Dar alipofanya ziara ya ghafla kwenye dampo hilo.(Picha na Zainul Mzige
wa MOblog).
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka halmashauri ya jiji, Bi. Enezael
Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya taka yanavyomwaga taka katika
dampo kuu taka la Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati wa ziara ya Mkuu wa
mkoa wa Dar.
Mkuu
wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa agizo mara moja kwa uongozi wa
Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha
miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka
katika dampo hilo. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Ndg. Raymond Mushi(mwenye suti nyeusi).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tirima Enterprises, Bw. Robert Ngeleshi akizungumzia
changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar
ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo.
Mkuu
wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick aliyeambata na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Ndg, Raymond Mushi wakiondoka eneo la tukio mara baada ya
kuhitimisha zoezi la kukagua miundo mbinu ya Dampo la taka la Pugu
Kinyamwezi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael Mshanga.
Na. Damas Makangale, MOblog
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ametoa agizo mara moja kwa
uongozi wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha
miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka
katika dampo hilo. MOblog inaripoti
Akizungumza
na baadhi ya viongozi wa wilaya na jiji hivi karibuni baada ya kufanya
ziara ya ghafla katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa
Mkoa amesema tatizo la miundombinu ya barabara kuelekea katika Dampo la
Pugu Kinyamwezi linasababisha foleni kwa malori ya kusomba taka katika
jiji la Dar.
“mara
ya mwisho wakati nakuja hapa kukagua hili dampo kulikuwa na taa na kazi
ilikuwa inafanyika usiku na mchana sasa kumetokea nini,” alihoji Mkuu
huyo wa Mkoa
Sadick
aliagiza kwa viongozi wa jiji kushughulikia haraka tatizo la
miundombinu ya barabara kuelekea Dampo ili kuongeza tija katika kazi ya
kumwaga na kusomba taka katika jiji la Dar es Salaam.
Alisisitiza
kwamba utaratibu mbovu wa umwagaji taka na miundombinu mibovu katika
Dampo la Pugu Kinyamwezi vinasababisha mrundikano wa taka katika
manispaa zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.
Amesema
kwamba ni muhimu kwa viongozi wa jiji kupata nguvu kazi ya kutosha ili
kuwe na watu watakaosimamia umwagaji wa taka wakati wa usiku ili
kudhibiti madereva wakorofi wanaomwaga taka ovyo bila kuzingatia
taratibu.
Sadick
aliongeza kuwa watendaji wa jiji ni lazima wawe na utaratibu wa kutoa
mafuta kwa wakati kwenye magari ya kusomba (Bull Dozer) na vitendea kazi
vingine.
Wakati
akitembelea maeneo kadhaa kati kati ya jiji kuanzia soko la Kisutu na
mitaa ya Libya, Mkuu wa Mkoa aliagiza mamlaka zinazohusika kushughulikia
haraka tatizo la maji machafu kupunguza harufu na kuzuia magonjwa ya
mlipuko.
“nawaagiza
mkae pamoja na mje na mpango mkakati utakaowezesha kumaliza tatizo la
maji machafu yanayotoka katika mitaro na mifereji ya maji machafu katika
ya jiji,” aliongeza
Wakati
huo huo, wadau kadhaa wa usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam
wameomba serikali kutoa kipaumbele kwa Dampo la Pugu Kinyamwezi na
kulitengea bajeti ya kutosha ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
No comments:
Post a Comment