Klabu ya Barcelona imeiambia Manchester United kuwa haina nia ya kumuuza nyota wake Cesc Fabregas.
Manchester United, imethibitisha kuwa
iliwasilisha tena ombi la kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni
milioni thelathini, lakini ripoti zinasema kuwa ombi hilo limekataliwa.Rais wa Barcelona Sandro Rossel, amekariri kuwa klabu hiyo haina nia ya kumuuza mchzaji huyo kwa klabu yoyote.
Kocha wa Manchester United, David Moyes amenukuliwa akisema huenda wasifanikiwe kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo Moyes amekiri kuwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward, angali anafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa wamemsajili mchezaji huyo.
Mara ya kwanza United iliwasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Barcelona.
Barcelona haijatoa taarifa yoyote, lakini kuna habari kuwa huenda matatizo yanayokumba klabu hiyo kwa sasa yamechangia pakubwa uamuzi huo kukataliwa.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Haijulikani ikiwa uamuzi wa Chelsea wa kutaka kumsajili mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney umechangia klabu hiyo kutaka kumsajili Fabregas
No comments:
Post a Comment