Dar es Salaam. Kampuni ya
Equator Suma JKT yenye ubia na Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la
Kujenga Taifa, imesaini mkataba na kampuni ya Farmer kutoka nchini
Poland utakaowezesha uzalishaji wa matrekta Tanzania.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo jana
jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Equator Suma JKT, Ramesh Patel
alisema kuwa mradi huo unagharimu Dola 70 milioni (Sh112 bilioni) ambazo
ni mkopo kutoka Poland.
“Kwa muda mrefu, Serikali imekuwa ikizungumzia
maendeleo ya kilimo, sisi tumeliona hilo na tulikuwa na mazungumzo na
Kampuni ya Farm ya Poland,” alisema Patel na kuongeza:
“Leo ni siku ya kihistoria, kwani tunatia saini
mkataba huu kuonyesha kuwa tuko tayari kuzalisha matrekta hapa nchini na
yataitwa kwa jina la Kitanzania.”
Alisema mradi huo utaanza kwa kuzalisha matrekta
machache ambayo yatafanyiwa majaribio na Kituo cha zana za kilimo na
teknolojia vijijini (Carmatec) cha Arusha ili kuyathibitisha kwa ubora
wa kimataifa.
Kwa upande wake, mwakilishi wa kampuni ya Farm
kutoka Poland, Robert Parcia alisema kuwa wameichagua Kampuni ya Equator
Suma JKT kutokana na ufanisi wake katika kilimo.
“Leo ni siku ya furaha kwetu kwani tumeingia
kwenye hatua mpya. Tunatarajia kwanza kuunganisha matrekta 1,200 kwa
mwaka na hiyo itaanza mwaka 2017. Yatakuwa matrekta ya kiwango cha juu
na ubora wake utakuwa ni kama wa Ulaya,” alisema Parcia na kuongeza:
“Tunashukuru kwa kuwa Serikali ya Poland imetupa msaada wa kifedha ndiyo
maana tunapata uhakika wa mafanikio.”
Naye Mkurugenzi wa Equator Suma JKT, Robert Ndege
alisema matrekta hayo hayatakuwa kwa soko la Tanzania tu, bali kwa
Afrika nzima.
“Wameichagua Tanzania kwa sababu ya uzuri wa eneo
la kibiashara. Tutazalisha matrekta, siyo kwa soko la Tanzania tu, bali
kwa Afrika nzima. Lengo letu ni kuhamisha teknolojia hiyo, ikiwezekana
asilimia 70 itengenezwe kwao na sisi asilimia 30,” alisema.
“Matrekta hayo yatakuwa yakitolewa kwa mkopo na
tutachagua mojawapo ya benki, ambapo watu wataomba mikopo na kuirejesha
hukohuko benki.”
Alisema kuwa mradi huo utakuwa endelevu na hautaishia tu kuzalisha matrekta bali utakuwa pia ukizalisha magari aina nyingine.
“Kiwanda hiki kimeanzishwa kwa ajili ya uzalishaji
wa matrekta, lakini tutazalisha na magari mengine. Tunategemea
kuendelea na uzalishaji kwa zaidi ya miaka 200 ijayo,” alisema Ndege na
kuongeza:
No comments:
Post a Comment