Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, January 16, 2014

MWANANCHI; MUUWEKEZAJI KAPUNGA RICE ANATUKODISHA MASHAMBA

 

Mbeya. Hivi karibuni wananchi wilayani Mbarali walilalamikia kitendo cha kukodishwa mashamba ya kulima mpunga kwa masharti magumu yanayotolewa na Mwekezaji wa Kampuni ya Kapunga Rice Project Limited.
Mwishoni mwa mwaka jana walimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwamba kampuni hiyo inakodi mashamba kwa  masharti magumu ambayo yanamnyonya Mtanzania kwa kiasi kikubwa. Kauli yao pia ilirudiwa Januari 7, mwaka huu ambapo walimweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa Kijiji cha Kapunga kwamba kampuni hiyo imerudisha ubepari nchini.
                        Aina ya kwanza ya ukodishaji na masharti yake
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga Ramadhan Nyoni alisema mbinu ya kwanza ya ukodishaji ni ile inayoitwa kilimo cha pamoja kati ya mkodishaji na mwekezaji.
Utaratibu huu, unahusisha  kampuni kutoa huduma za mbegu ya kupanda, mbolea ya kukuzia DAP, mbolea ya kukuzia UREA na  SA\, mbolea ya kuzalishia MOP, kutengeneza shamba ,kuvuruga, inalipia gharama ya upandaji, kung’olea magugu, dawa, kupiga dawa  na kuvuna.
Mkodishaji yeye kazi yake ni kuhakikisha anahudumia shamba kwa kutafuta vibarua wa kutosha na kazi inafanyika kwa muda uliopangwa. Kwa kawaida mwananchi hahitaji mtaji mkubwa kuwekeza sababu asilimia 97 ya gharama zote inalipwa na kampuni.
Lakini mkataba wake bila  kujali ni mpunga kiasi gani umepatikana katika kila shamba, kampuni inavuna na kuchukua mpunga kwa ajili ya kujilipa gharama zote ilizozitumia, kulingana na kiwango ilichokiweka.
Kwa mfano mwaka 2013, kila shamba moja la ekari 15, kampuni inachukua  tani 39 au magunia 390 ya mpunga na kwamba mpunga uliobaki mfano tani saba au magunia 70, kampuni  tena ilichukua asilimia 60 ya mpunga huo na asilimia 40 ya unaobaki alichukua mwanachi.
Nyoni alisema pia kwamba kama shamba husika litazalisha tani 39 zinazohitajika na kampuni, basi mkulima hawezi kuambulia chochote kwani kampuni ilichukua magunia yote.
Utaratibu huo ulitajwa kuwa ni mbaya  kutokana na ukweli kwamba haulengi kumsaidia mkulima bali kuinufaisha kampuni kwani yakitokea mabadiliko ya tabianchi, basi mkulima hawezi kupata hata mpunga wa chakula.
                          Aina ya pili ya ukodishaji na adha yake
Utaratibu mwingine wa kukodi shamba uliopo kwenye Kampuni ya Kapunga Rice Project Limited ni ule wa kilimo cha wakulima wa nje.

No comments:

Post a Comment