Polisi nchini Afrika Kusini
wamesema kuwa aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa Rwanda, Patrick
Karegeya, amepatikana ameaga dunia katika hoteli moja mjini
Johannesburg.
Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Karegeya alipokonywa cheo cha kanali baada ya
kutofautiana na mshirika wake wa zamani, rais Paul Kagame wa Rwanda,
ambaye alimshutumu kwa kuhusika na mashambulio ya kigaidi mjini Kigali.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari,
na chama cha upinzani cha Rwanda National Congress, RNC, inasema kuwa
Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.
Hata hivyo mamlaka nchini Afrika Kusini haijathibitisha madai hayo.
No comments:
Post a Comment