Ndege
ya Zan Air ikiwa kichakani kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume kisiwani
Pemba. Picha ndogo ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakari
Khamis Bakari.
Waziri
wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakari Khamis Bakari, pamoja na abiria
17 wamenusurika kifo, baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zan air’
waliyokuwa wanasafiria kupata matatizo ya breki na kusererekea
vichakani.
Ndege
hiyo iliyokuwa na marubani wawili, iliserereka wakati inatua katika
Uwanja wa Ndege wa Karume kisiwani Pemba ikitokea Unguja juzi jioni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa Kusini Pemba, Swalehe Mohamed Swaleh, akizungumzia ajali
hiyo alisema ilitokea baada ya ndege hiyo kuwasili Pemba ikitokea
Unguja.
Alieleza kuwa ilikwenda kwa kasi kama kawaida ikitarajiwa kuwa ingepunguza mwendo lakini ilishindwa kufanya hivyo.
CHINI Alieleza kuwa ilikwenda kwa kasi kama kawaida ikitarajiwa kuwa ingepunguza mwendo lakini ilishindwa kufanya hivyo.
“Ni
kweli ndege hiyo ya ‘Zan Air’ ilipata hitilafu na kuingia majanini
lakini abiria wote waliokuwamo na marubani wawili, walitoka
salama,’’alifafanua.
Alisema polisi imeliimarisha ulinzi wa ndege na abiria hao na haikuruhusiwa watu wasiohusika kuzengea eneo hilo.
Baadhi
ya mashuhuda walioishuhudia ndege hiyo walisema ilikwenda kwa kasi
kubwa kama gari zinazofukuzana na kumfanya muongoza ndege uwanjani hapo
kukaa pembeni akishangazwa na kilichotokea.
Walisema baada ya kuiona ikiwa haipunguzi mwendo kasi kama inavyotakiwa, ghafla iliingia majanini na kuacha barabara ya ndege.
Mkuu
wa kikosi cha zima moto na uokozi kisiwani Pemba Shaban Zidi Heri Juma,
alishuhudia ndege hiyo ikikimbia kwa kasi kubwa ambapo gari la zima
moto liliifuata kwa haraka hadi iliposimama kichakani.
Meneja
wa uwanja huo, Rajabu Ali Mussa, alisema tukio hilo lilitokea saa
10:30 jioni jana na kwamba ilipata hitilafu baada ya uchunguzi wa awali
kuonyesha matatizo ya breki.
Alifafanua kuwa wataalamu watachunguza ili kujua chanzo cha hitilafu kwenye breki.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment