Kutoka kulia ni Bw. Riziki Shaweji (Waziri wa Fursa,Mipango na
Uwezeshaji CBE-Dodoma),Bw.Ruge Mutahaba (Mkurugenzi Mtendaji Clouds
Media Group) na Bw. Alex Morio (Katibu Mkuu wizara Mipango na Uwezeshaji
CBE-Dodoma).
Wizara ya Fursa, Mipango na uwezeshaji wa serikali ya wanafunzi CBE
jana tarehe 28/12/2013 imeondoka na kuelekea Dar es Salaam kama sehemu
ya kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza na Wizara ya Habari,Waziri wa wizara hiyo Mhe, Riziki
Shaweji ambaye ameambatana na katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe. Alex Morio
amesema leo (29/12/2013) wamekutana na Bw. Ruge Mutahaba mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group
kwa lengo la kupata ushauri na maoni mbalimbali juu ya fursa kwa vijana
hususani kwa wasomi wa Elimu ya juu lakini pia kama wizara kutoa
mikakati iliyonayo juu ya fursa kwa wasomi wa Elimu ya juu hususani
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma , hata hivyo wizara hiyo imepata
fursa ya kuwasilisha Baadhi ya mikakati ikiwa ni pamoja na mkakati wa
CBE kuwa na maadhimio ya ''CBE Day'' siku ambayo itaambatana na matukio
mbalimbali, pia suala Maktaba kwa maana ya upatikanaji wa Vitabu
chuoni,Suala la Mr. na Miss CBE, pamoja na hayo wamebainisha umuhimu wa
uwepo wa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana wasomi katika mkoa wa
Dodoma.
Bw.Ruge Mutahaba (Mkurugenzi Mtendaji Clouds Media Group) akiwa katika moja ya Semina ya Fursa mkoani Tanga (October 2013)
Kwa upande wake Bw. Ruge Mutahaba amepongeza sana serikali ya wanafunzi
wa CBE kwa kubuni na kuwa na Wizara ya Fursa, Mipango na uwezeshaji na
kusema Mkoa wa Dodoma ni Mkoa wenye Fursa nyingi na wenye wasomi wengi
wa Vyuo vya Elimu ya juu, na hivyo ni mhimu sana kwa Taasisi za Elimu ya
juu kutumia Elimu yao kwa kuwa wabunifu na kuchangamkia Fursa zilizopo
ili kuleta chachu ya maendeleo katika jamii kwa ujumla.
Ikumbukwe kwamba Ruge Mutahaba amekuwa mstari wa mbele kupigania vijna
katika nyanja za uchumi kwa maana ya kuibua fursa zilizopo katika Mikoa
mbalimbali nchini Tanzania kwa lengo la kupambana na dhana ya ukosefu wa
Ajira kwa vijana.
Kwa upande wake Waziri wa fursa, mipango na uwezeshaji Mhe; Riziki Shaweji "amepongeza
hatua na mikakati pamoja na juhudi zinazoonyeshwa na Bw. Ruge Mutahaba
kwa kuwa na nia ya dhati ya kuwakomboa vijana kwa lengo la kupunguza
suala la ukosefu wa ajira nchini" Waziri huyo ameongeza kwa
kusema Wizara ya Fursa imejipanga kuibua na kufungua milango kwa
wanafunzi wa chuo hicho kuchangamkia Fursa zilizopo Mkoani Dodoma ili
kuleta chachu kwa wasomi wa vyuo vya Mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa
ujumla .
Kuna kila sababu ya wasomi kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazoonyeshwa
na wadau kama Ruge Mutahaba kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Bw. Riziki Shaweji (Waziri wa Fursa,Mipango na Uwezeshaji CBE-Dodoma)
Bw. Alex Morio (Katibu mkuu wa Fursa,Mipango na Uwezeshaji CBE-Dodoma) akiwasilisha mikakati ya wizara yake kwa Bw, Ruge Mutahaba (Mkurugenzi Mtendaji Clouds Media Group)
Bw. Riziki Shaweji (Waziri wa Fursa,Mipango na Uwezeshaji
CBE-Dodoma) akiwasilisha mikakati ya wizara yake kwa Bw, Ruge Mutahaba
(Mkurugenzi Mtendaji Clouds Media Group)
Mhe; Remidus M. EmmanuelRais wa Serikali ya Wanafunzi - CBE - Dodoma
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Campus CBE - Dodoma Mhe; Remidus M. Emmanuel.Amepongeza utendaji wa wizara ya Fursa,Mipango na Uwezeshaji na kuongeza kuwa umefika wakati kwa wasomi wa Taasisi za elimu ya juu kuangalia namna bora ya kupunguza changamoto ya ajira nchini. "Tayari kama serikali ya wanafunzi tuko katika muendelezo wa kuchangamkia Fursa ya ufugaji nyuki katika Wilaya ya Chamwino kwa ushirikiano mkubwa wa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Fatma Ally.
"Inapendeza kama serikali ya wanafunzi inapokuwa mfano kwa wanafunzi hatua ambayo italeta mapokeo chanya kwa wanafunzi wote kwa kuthubutu na kuchangamkia fursa kwa kuiga mfano wa viongozi wao"
Alisema Rais huyo na kusema kuwa anaamini kila kitu kitawezekana kupitia wizara yake ya fursa, mipango na uwezeshaji, kwa kuchangamkia fursa zilizoko mkoani Dodoma kwa Maendeleo ya CBE na Taifa zima kwa ujumla .
Pia amepongeza juhudi zinazofanywa na Bw. Ruge Mutahaba kupitia kampuni yake ya Clouds Media Group na kuitaka jamii ya wasomi wa vyuo vyote nchini kumuunga mkono kwani juhudi zake zinalenga maslahi ya vijana wa Taifa zima la Tanzania.
No comments:
Post a Comment