Hatimaye mashindano ya Mahimbo Cup yazinduliwa rasmi leo hii katika viwanja vya Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma,na hicho ni kikosi cha timu ya Diploma 2 kilichomenyana na vijana wa Bachelor one.
Kikosi maridadi cha Diploma 2 kikiongozwa na mshambuliaji matata Salala aliyezifumania nyavu za Bachelor one mara mbili na kuipa timu yake ushindi,huku safu ya ulinzi ikiongozwa na beki kisiki Juma alimaarufu Mbuyu Twite.
kikosi cha Bach one kikiwa tayari kukaguliwa ili kuanza kutupa karata yao ya kwanza dhidi ya Diploma two,ambapo walipoteza mchezo huo.
mwamuzi akijiandaa kukagua timu zote kabla ya kipute kuanza.
Shukrani uongozi wa Chuo kwa kutoa vifaa vipya vya michezo,hakika ni sura mpya kwa mashindano haya.
Mshauri wa wanachuo akiteta jambo na Mkuu wa Chuo.
Naibu waziri wa michezo yuko makini ili mambo yaende sawa,na Mh.Rais akifuatilia hatua kwa hatua.
Vikosi vya timu zote kabla ya kumenyana.
Mh.Rais akizungumza na wachezaji wa timu zote kabla ya mashindano kuanza,ambapo aliwataka kudumisha amani na kuyafanya mashindano kuliakisi jina la Mahimbo lililobeba jina la mashindano hayo.
Tumefarijika na uwepo wako katika ufunguzi wa mashindano yaliyobeba jina lako.
Upendo na amani ni nguzo katika mashindano haya,hizo ni nasaha toka ktk uzinduzi wa Mahimbo Cup.
Mkuu wa chuoMh.Mahimbbo akipiga penalt kuashiria kuanza kwa mashindano ya Mahimbo Cup,ambapo alimpeleka mlinda mlango sokoni na kutingisha nyavu.
Naibu katibu wa wizara ya mawasiliano Comrade Theo akimhoji Captain wa timu ya netboll Bi Saada Tamimu juu ya mashindano,ambapo alitupa kilio chake kwa mashabiki pia kutupia macho michezo mingine kuliko kuutazama kabumbu pekee.
Ni mshikemshike katika lango la Bacherol one huku mlinda mlango akijiandaa kuokoa dhoruba langoni mwake.
Kashikashi inaendelea katika lango la Bach one,hakika safu ya ushambuliaji ya Dip 2 haikuwa butu.
Bw.Steve Shinji akikabidhi jezi kwa Captain wa team ya netball kabla ya mashindano kuanza
No comments:
Post a Comment