Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Saturday, November 2, 2013

MTOTO WA NYOKA NI NYOKA MUONE MTOTO WA DAVID BECKHAM NDANI YA MANCHESTER UNITED.


David Beckham na watoto
Taarifa ikufikie kwamba kwenye headlines sasa hivi, club ya soka ya Manchester United imetajwa kuwa kwenye mipango ya kumchukua mtoto wa kwanza wa David Beckham aitwae Brooklyn ili ajiunge na Academy ya club hiyo.
Unaambiwa makocha wa Manchester United wamekua wakitazama uwezo wa soka wa Brooklyn mwenye umri wa miaka 14 na huenda akaalikwa kujiunga na Academy ya club hii ambayo baba yake alitokea kwenye mechi zinazocheza kwenye 400, kushinda Premier League mara sita, FA Cup mara mbili pamoja na European Cup.
Brooklyn ambae alikua kwenye academy ya LA Galaxy Marekani wakati wa time ya baba yake ameshaingia kwenye headlines za kuwa karibu na club kama Chelsea na Queens Park Rangers.
Hapa ni wakati watoto wote watatu wa kiume wa Beckham walipoalikwa kwenye mazoezi na timu ya PSG
Hapa ni wakati watoto wote watatu wa kiume wa Beckham walipoalikwa kwenye mazoezi na timu ya PSG
David Beckham ambae aliondoka Manchester United 2003 kwenda Real Madrid, wiki hii alimpeleka mwanae kwenye viwanja vya mazoezi vya Manchester United Carrington ambapo huku mipango mingine ikiendelea, magazeti la Ulaya yanaripoti kwamba Manchester United inatarajiwa kusema chochote kama itamchukua na kumpa nafasi kwenye timu ya watoto au la.
d 1 cruz akiwa psg alikoalikwa kwa mazoezi
Kwenye moja ya interview zake, Beckham alipoulizwa kuhusu watoto wake kuwa wachezaji alisema ‘kama mzazi siku zote una wasiwasi, je watakua na njaa ya mafanikio kama niliyokua nayo? na kila baada ya kucheza huwa wananiuliza, baba nimecheza vizuri?’

No comments:

Post a Comment