MKOA
wa Morogoro na vitongoji vyake kwa sasa umegubikwa na simanzi kubwa
baada ya watu watano wa familia moja kufariki kwa mpigo katika ajali ya
gari.
Happiness Mwakyami.
Ajali
hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Cardina, yenye namba za
usajili T 180 AWT na Fuso namba T324 AWL lililokuwa likiendeshwa na John
Mombozi likitokea Dar es Salaam, ilitokea Oktoba 13, 2013, eneo la Visiga, Kibaha mkoani Pwani.
Jeneza la Happiness Mwakyami.
NI MHADHIRI WA SUA
Watu
waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Kilimo Sokoine (SUA) aitwaye Mwaitulo Suma Andalwisye aliyekuwa dereva
wa gari ndogo na wanawe watatu; Gamalieli Mwakyami, Happiness Mwakyami
na Jeremy Mwakyani pamoja na mtumishi wao wa ndani, Elita Mpagama.
Simanzi imeivaa familia hiyo ambayo
kwa sasa imebaki na baba tu aitwaye Jimmy Wilson Mwakyami, mwajiriwa wa
Kiwanda cha Sukari Kilombero, Morogoro ambaye ni Injinia.
Elita Mpagama.
IDD YA BALAA
Habari
zilizopatikana eneo la msiba zinasema kwamba, Bi. Mwaitulo (36) alikuwa
akielekea jijini Dar es Salaam ambapo angeiacha familia yake nyumbani
kwa mama yake mdogo, Sister Mwakatogo ili wale Sikukuu ya Idd wakati
yeye akiwa safarini Kampala, Uganda kikazi.
Ilielezwa
kuwa, kwa sababu mumewe alikuwa kazini Kilombero, walikubaliana
aichukue familia hadi Dar kwa bibi yao ili aiche hapo halafu yeye
aendelee na safari yake ya Uganda.
“Huyu dada
jamani ananiuma sana...unajua alipata safari ya kikazi kwenda Kampala,
sasa akaona si busara kuwaacha watoto peke yao nyumbani, baada ya
kushauriana na mumewe ndiyo akaamua kuwachukua akawaache kwa bibi yao,
akirudi awapitie - kumbe Mungu alishapanga yake.
Suma Mwakyami.
“Inauma
sana. Mimi namuonea huruma zaidi huyo mumewe. Inahuzunisha sana.
Kuondokewa na familia nzima siyo jambo dogo. Mungu atamwekea wepesi na
kumpa moyo wa ustahimilivu,” alisema jirani mmoja kwa sharti la
kutoandikwa jina lake kwa kuwa si msemaji wa familia.
Jeneza la Suma Mwakyami.
SIMULIZI YA MAJONZI
Kati
ya mambo yaliyozidisha majonzi katika ibada ya kuwaombea marehemu hao,
Oktoba 15, mwaka huu nyumbani kwao, Sua mjini hapa ni namna ndoto za
watoto waliofariki pamoja na mama yao zilivyozimika kama mshumaa kwenye
upepo mkali.
Mtoto wa kwanza katika familia hiyo,
Gamalieli (8) alikuwa anasoma darasa la nne katika Shule ya St. Marry’s
mjini hapa, Happiness (5) alikuwa chekechea na Jimmy akiwa na umri wa
miaka miwili tu wakati mtumishi wao wa ndani akiwa na miaka 18.
KIU YA ELIMU
Mhadhiri huyo alikuwa mama bora wa kuigwa katika familia za
Kitanzania kwa kuwa alikuwa akipigania sana elimu. Kabla hajaanza kazi
chuoni hapo, alipata elimu yake hapohapo, pia hadi mauti yanamkuta
alikuwa akiendelea kusoma.
Mwaka 1999 alijiunga chuoni hapo akitokea Shule ya Sekondari Loleza,
Mbeya ambapo alihitimu Shahada ya Kwanza katika Kilimo cha Bustani
‘Bachelor of Science in Horticulture’ mwaka 2003 na kuajiriwa hapohapo
kama Mhadhiri Mkufunzi.
Katika kujiendeleza zaidi mwaka 2007 alianza masomo ya Shahada ya
Uzamili katika Mimea na Vipando ‘Master of Science in Crop Science’
ambapo alihitimu mwaka 2009 – akapandishwa cheo na kuwa Mhadhiri kamili.
Mpaka mauti yanamkuta alikuwa akisaka Shahada ya Uzamivu ‘Doctor of Philosophy – PhD’ chuoni hapo.
BABA ASHINDWA KUZUNGUMZA
mume wa marehemu Mwaitulo, Jimmy (mwenye shati ya michirizi) ambaye
ajitihadi kujikaza na kupita mbele ya majeneza yote huku machozi
yakimbubujika.
Ijumaa lilitaka kuzungumza naye mawili matatu kuhusiana na namna
alivyoupokea msiba huo, lakini hakuweza kutokana na kuzidiwa na huzuni.
SAFARI YA MBEYA
Kaimu Mkuu wa SUA, Utawala na Fedha, Profesa Jayro Matovelo alisema
chuo kimepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kwamba marehemu alikuwa
mchakapazi sana.
Baada ya ibada na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu hao, msafara
wa kuelekea nyumbani kwao, Kyela, Mbeya ulianza mishale ya saa 9 alasiri
No comments:
Post a Comment