Serikali ya Kenya kupitia kwa
waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki
katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na
wengine 175 kujeruhiwa.
Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi
walio ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani
ikiwa wanwazulia waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu
mbali mbali z jumba la Westgate.
Shirika la Red Cross awali katika
taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50
kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi
Jumamosi mchana.
Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la
Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab
wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika
ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu
wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.
Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na
ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo
huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali
wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.
Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao
kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha
kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne
na kuwpaiga watu risasi kuholela.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki
ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa
Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale
waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa
zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa
walifariki kutokana na majeraha yao.
No comments:
Post a Comment