Rais wa Ufaransa Francois
Hollande, amekiri ukatili uliotekelezwa na taifa lake wake wakati
ilipokuwa ikitawala Algeria wakati wa ukoloni, lakini hakuomba msamaha.
Akiongea kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yake
nchini Algeria, kama rais wa Ufaransa, rais Hollande, aliliambia bunge
na nchi hiyo kuwa ''anatambua mateso na dhuluma ambazo zilisababisha na
ukoloni dhidi ya raia wa Algeria''.Lakini rais huyo wa Ufaransa, aliongeza kuwa hakuja nchini humo kuomba msamaha.
Maelfu ya raia wa Algeria, waliuawa wakati wa vita vya uhuru wa taifa hilo vilivyodumu kwa muda wa miaka saba.
Je rais wa Ufaransa ataomba msamaha?
Hata hivyo raia wengi wa Ufaransa, pia waliuawa wakati wa vita hivyo baada ya raia wa Alheria kuwashambulia kulipisa kisasi kabla ya Algeria, kupata uhuru wake mwaka wa 1962.
Rais Hollande, amesema kunahaja ya kusema ukweli na kutambua kuwa haki za raia wa nchi hiyo zilikiukwa.
Amesema Ziara yake imefungua awamu mpya ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ambazo ni sawa.
Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Algeria, miaka mitano iliyopita, mtangulizi wa rais Hollande, Rais Nicolas Sarkozy, pia alikiri kuwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa wa miaka 132 ulisababisha maafa na dhuluma nyingi dhidi ya raia.
Sawa na rais Hollande rais Sarkozy hakuomba msamaha.
No comments:
Post a Comment