Na Mwandishi Wetu
Vipindi vya
televisheni vya shindano la Maisha Plus
kuanza kuonyeshwa leo usiku katika kituo
cha televisheni, TBC1.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar, Mratibu wa Mashindano hayo, Masoud Ali ‘Kipanya’
alisema vipindi hivyo vitaonyesha hatua za awali ambazo ni usaili na mpaka
kupatikana kwa washiriki 30 waliobahatika kuingia kijijini.
“Tutaanza
kuwaonyesha kipindi chetu kuanzia leo hii saa nne na dakika tano usiku, kipindi
kitaanza kwa kuonyesha hatua za mwanzo kabisa za mashindano haya,” alisema
Kipanya.
Alifafanua
akisema kuwa vipindi 10 vya mwanzo
vitaonyesha mchakato mzima wa upatikanaji wa vijana 18 kutoka Tanzania watakao
ungana na vijana wengine 12 kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi zitakazotoa
washiriki watatu kwa kila nchi.
Usaili wa mwaka huu
ulikuwa tofauti na miaka mingine ambapo orodha ya washiriki 40 ilitengenezwa na
ikagawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lilikwenda mkoani
iringa kuishi kwenye vijiji vya huko na kushiriki shughuli za kijamii.
Kundi la Pili
litaenda visiwani Zanzibar ambalo pia litashiriki utamaduni wa kila siku wa
kimaisha wa visiwani humo ambapo ni washiriki tisa tu katika kila kundi
watachukuliwa na watachujwa kutokana na jinsi walivyoyamudu maisha ya huko.
“Vijana wakiwa huko
katika vijiji vya kweli watakuwa wakishiriki shughuli za kilimo, usafi, za
kiafya na nyinginezo kabla hawajaingia katika kijiji cha Maisha Plus”,
alifafanua Kipanya.
Baada ya kundi la
kwanza na la pili kutoa washiriki tisa kila kundi, washiriki 18 watakuwa
wameshapatikana, na sasa nchi za zikishapata washiriki wake 12, idadi ya
washiriki 30 itaingia kijijini cha Maisha Plus katikati ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment