Marais wa Taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu vya Dodoma leo
(09/03/2014) wametoa yao ya moyoni wakati wakishiriki kampeni ya
kufanya usafi iliyoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Elimu
ya Biashara CBE -Dodoma.
Viongozi hao wamesema mara nyingi vyuo vyao vimekuwa vikitumika
visivyo katika jamii hatua inayopelekea mtizamo hasi dhidi ya vyuo
hivyo kutoka katika jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi ya CBE Mhe. Remidius
Emmanuel amesema " Taaluma ya habari inapaswa kuheshimiwa na kila kada
, wapo baadhi wa wamiliki wachache wa baadhi ya Blogu wamekuwa
wakitumia Blogu hizo kuchafua vyuo hivyo hatua ambayo inaleta mtizamo
hasi katika jamii,. Mfano Mwaka jana (2013) ipo baadhi ya mitandao ya
kijamii (Blogu) ziliwaonyesha baadhi ya vijana wakifanya vitendo vya
ngono kwa ku- ect picha hizo na kisha waandishi wa habari hiyo
walidai kuwa vijana hao ni wa CBE kitu ambacho si kweli na hawakuwa
vijana (wanafunzi) wa CBE . Upotoshaji huo umekuwa ukileta madhara
kwa chuo lakini pia kuharibu sifa na dhana ya kukubalika kwa
kiwango cha elimu katika vyuo vyetu. Aliongeza kwa kusema Serikali
inapaswa kuweka taratibu za kuwachukulia hatua baadhi ya Wamiliki wa
Blogu wanao tia doa tasnia hiyo nyeti ya habari. Ikumbukwe kwamba
Blogu ni chombo chenye heshima zake na watu wanaishi na kuendesha
maisha yao kupitia Blogu, hivyo sio vema watu wachache waharibu taswira
ya mitandao hiyo ya kijamii kwa kupotosha umma na kujenga dhana
potofu na mitazamo dhidi ya uwepo wa Blogu hizo" Alisema Rais huyo wa
CBE Dodoma.
Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi Chuo kikuu ca Dodoma Bw. Mahamudu Rashid Hussein
Kwa upande wake ,Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi Chuo kikuu ca
Dodoma Bw. Mahamudu Rashid Hussein amesema ifike wakati jamii
ijenge tabia ya kuyazungumzia na mazuri yanayofanywa na vyuo
/wanavyuo badala ya kujikita katika mlengo wa kuvichafua vyuo na
taaluma yake. Amesema , Hakuna chuo ambacho kinaunga mkono ukiukwaji
wa maadili kwani kila chuo kinazo taratibu na sheria zake za kulinda
Maadili ya chuo husika. Lakini inapotokea mtu akaamua kutumia jina
la chuo katika mtizamo hasi kwa maana ya kujipatia idadi kubwa ya watu
wanaotembelea Mitandao ya kijamii (Blogu) au kwa maana ya kuuza sana
magazeti kwa habari ambazo hazina ukweli ni kupotosha jamii na
kuharibu sifa za vyuo. Ni vema taaluma ya habari ikaendelea kulindwa
kwa kutoa habari yenye ulinganifu (Ku - Balance habari) na ukweli
kutoa vyanzo fasaha. "Sio mtu anapiga/kuchukua picha chafu katika
mitandao alafu anasema ni wanafunzi wa vyuo "Alisema Rais huyo .
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo St. John Bw. Katumbi Edmund J. Akizungumza na Vyombo vya Habari.
Katika hatua nyingine Rais wa Chuo kikuu cha St. John Mhe Katumbi
Edmund J. amesema vyuo vikuu vitaendelea kutoa huduma mbalimbali
katika jamii na kuongeza kuwa ni vema jamii ikaendelea kutoa
ushirikiano pale wanavyuo wanaposhiriki katika huduma za kijamii.
Bw. Katumbi amesema anashangazwa na dhana ya kwamba wanafunzi wa vyuo
wamekuwa wakijiuza kwa Tsh. 500, Amesema hiyo ni fedheha na aingii
akilini kwa mwanachuo ambaye analipa Mamilioni ya fedha katika Elimu
yake alafu aende akajiuze kwa Tsh 500 hizi ni dhana potofu za uongo
ambazo hazipaswi kuvumiliwa.
"Nashangaa kwa nini mambo mazuri hayaandikwi na badala yake
tumekuwa tukiandikwa na kusomeka katika mtizamo hasi kwenye jamii,
hivyo niiombe jamii iwachukulie wanavyuo kama watu wenye nia
njema na wako tayari kushirikiana na jamii husika katika kuzitumia
taaluma zao kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
No comments:
Post a Comment