Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Sunday, February 23, 2014

KIJANA MAHILI KUTOKA CBE DODOMA ANG'AA NDANI YA MAISHA PLUS IRINGA.......SOMA HAPA

 Bw. Dotto Nkoronko mwanafunzi wa Diploma II CBE Dodoma 
Form zilikuja chuoni kwetu tarehe 05/1/2014  na kukusanywa tarehe 24/1/2014 ulikua mwisho, na mshiriki ambae anaiwakilisha sumbawanga akiwa mikonon mwa Chuo cha CBE mahali alipochukulia form mshiriki pekee toka CBE Dotto anakwenda Ukilosha Sumbawanga katika mashindano ya Maisha Plus na amepangiwa kambi ya kijiji cha iringa anaitaji ushiriki Wako katika kumuwezesha kushinda taji la maisha plus kama mtanzania na mwana  CBE Dodoma

Kijana huyu  anazaliwa katika kijiji cha Laela wilayani Sumbawanga vijijini huko mkoani Rukwa ni watoto waliozaliwa mapacha huku mama mzazi wa mapacha hawa akifanya maamuzi ya kuwapa majina kwa lengo la kuwatofautisha wanawe, mmoja ambaye ni Kulwa anapewa jina la MUHANYI na Dotto akipewa jina la MBONIMPAYE maana ya majina haya ni MUNGU AMENIPA ikiwa kama shukran kwa mwenyezi mungu, Mama mzazi wa kiongozi huyu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mwalimu wa shule ya  msingi na baba yake akiwa mganga wa hospitali ya kijiji hicho, Ndipo wanapo amua kumlea mtoto wao katika hekima na kimo akimpendeza mungu na wanadamu pia, kiongozi huyo alizaliwa tarehe 14/06/1990 ambaye ni chotara wa kabila la kiha kutoka mkoani Kigoma (kabila la baba) huku kabila la mama likiwa ni fipa kutoka mkoani Rukwa. Familia hii ni ya imani ya dini ya kisabato na ni familia ya watoto wanne na wote ni WAKIUME tu wa kwanza akiitwa MIGISHA, wa pili MINZERO na watatu na mwisho ni MUHANYI na MBONIMPAYE  yaani (Kulwa na Dotto).

   Mbonimpaye ambaye ni miongoni mwa wabunge katika bunge la wanafunzi CBE Dodoma , safari yake ya maisha katika siasa na mafanikio inapo anza kuchipua kama majani yaotayo juu ya uso wa dunia akiwa katika chuo cha elimu ya biashara tawi la dodoma. Je atafanikiwa???

Yeye binafsi anavyo amini (mbonimpaye) anasema:-

"Am Maisha ni kuendela  kutafuta hadi zamu yangu ya kushinda ifike, Sikatishwi tamaa na mtu yeyote yule na KUSHINDWA ndipo nitaona kuwa ugumu ni kipindi cha mapito kuelekea MAFANIKIO, maisha ni safari ndefu huwezi kuamini kama kuna mungu iwapo utabaki katika furaha milele bila kupitia shida ikumbuke JANA, itazame LEO, na itafakari KESHO
.
Je mama mzazi wa mbonimpaye anamzungumziaje?? (Mwl Sangu)
:-

Mara nyingi mwanangu huwa ananiambia hasa tunapokuwa tunakula chakula cha husiku kuwa "mama mimi siku moja nitakuwa kiongozi mkubwa" mimi na baba yake huwa tunabaki tukicheka tu lakini huwa naona sasa mwanangu amekuwa na hayo ndo maamuzi yake na ndo mana siwezi kumshangaa lakini namtakia mafanikio mema maana akifanikiwa yeye na mimi pia nitakuwa nimefanikiwa hata kama hatonipa pesa basi kwa heshma atakayo kuwa nayo kwa kipindi hicho itakuwa ni furaha kwangu, dotto ni mtoto wangu wa mwisho na ninampenda sana nimtakie mafanikio mema ila asisahau kama mungu yupo na ndiye mpangaji.
Kaka wa 1 wa mbonimpaye anasemaje?? (Migisha Nkoronko):-
Safari ya mdogo wangu kimaisha na hata kisiasa mimi binafsi naona barabara ya mafanikio yake bado ina mabonde, milima na hata kona zilizo nyingi sana hivyo ni muda wake tu bado haujafika
(maturity time).

Stopper (Manager wake):-
Duuu kiukweli dotto ni mtu wa kujaribu kila kitu na anaweza sana mara ya kwanza ninakutana nae ilikuwa kwa tamasha la ukimwi pale ndipo nilipomjulia dotto na tulimpa kazi ya Umc na aliweza sana hata pasipo majaribio ni mtu ambae ana focus mbele. Nimtakie mafanikio mema katika maisha yake
I dont stop when i'm tired I stop when i'm done
                           *******IN GOD WE TRUST*******   
Imendaliwa; na Serikali ya  COBESO DODOMA Kupitia  Bw.Ezekiel Mgaya (Stopper Jaga jaga)

AKIWA KATIKA MAANDALIZI YA SAFARI YAKE........ 










No comments:

Post a Comment