Dalili za
kifo zipo nje nje, zinajidhihirisha kwa ukaribu zaidi katika maisha ya
Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya, sababu
kuu ikiwa zigo la tuhuma za kumbaka na kumwambukiza Ukimwi
mwanafunzi.Siyo Kapuya tu, hata mwanafunzi anayedai kubakwa na waziri
huyo wa zamani, naye maisha yake siyo salama, kwa hiyo rai imetolewa kwa
wote wawili kupewa ulinzi stahiki.
Tuhuma kuu ni
Kapuya kuripotiwa na gazeti pamoja na mitandao kadhaa ya intaneti,
akidaiwa kumbaka mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 16 (jina
tunalihifadhi), anayesoma Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni, Dar es
Salaam.
Mwanafunzi huyo amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa
alibakwa mara mbili na Kapuya kisha kuambukizwa Ukimwi wakati
alipokwenda kumuomba msaada wa ada ya shule kwa sababu yeye ni yatima.
Mh. Juma Kapuya.
KAPUYA NA KIFO
Kapuya, aliye kiongozi mwandamizi wa Tanzania, akiongoza wizara
mbalimbali kama vile Elimu, Kazi, Vijana na Ajira, Habari, Utamaduni na
Michezo, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na kadhalika, maisha yake yapo
hatarini kwa sababu zifuatazo;
MOSI; Wananchi
waliozungumza na Risasi Jumamosi, wamesema kuwa hatari ya kwanza ni SMS
ambayo inadaiwa Kapuya aliituma kwa mwanafunzi huyo akimtishia kumuua.
“Kapuya ni
kiongozi mwenye heshima kubwa nchini, kukumbwa na tuhuma za kutishia
kuua siyo dogo,” alisema Phabian Tarimo ambaye alidai ni jirani wa
mwanafunzi huyo na kuongeza:
“Inawezekana kujiepusha na aibu hiyo ya tuhuma za ubakaji au kutishia kuua, akaamua kujiua.”
PILI; Kingine ambacho kinaashiria hatari kwa maisha ya Kapuya ni SMS
ya kutishia kujiua ambayo inadaiwa kiongozi huyo alimtumia denti
mlalamikaji.
Vyanzo vyetu
vinasema, SMS hiyo kutoka kwa Kapuya inasomeka: “Nimewakosea sana, acha
nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.”
Mchangia
maoni mmoja wa mtandaoni, Lubelo Issa, alisema: “Kapuya kutamka kujiua
siyo jambo dogo, naamini anamaanisha, inabidi familia yake na marafiki
zake wawe karibu naye.
“Ikiwezekana hata polisi wawe macho, maana hilo ni kosa la jinai. Kwa
mtu mkubwa kama Kapuya kupewa tuhuma nzito kama hizo, ni rahisi
kumkatisha tamaa. Ni rahisi kuuona mwisho wake wa kisiasa.
“Hali yake mbele ya familia yake ipoje? Hayo mambo ni mzigo ambao unaweza kumpeleka mbali hadi kufikia hatua ya kujiua.”
DENTI NA KIFO
MOSI; SMS ambayo amedai kutumiwa na Kapuya ni hatari ya kwanza na
katika hilo, imeshauriwa na wananchi kwamba denti huyo alindwe usiku na
mchana.
“Kapuya amechafuka sana na ikiwa ni kweli zile SMS zimetumwa na yeye,
basi yule mtoto achungwe na alindwe kikamilifu. Kapuya amejenga heshima
yake kwa miaka mingi, hawezi kukubali kuchafuliwa kienyeji.
“Inawezekana
Kapuya akawa na moyo wa subira pamoja na huruma lakini wapo wapambe
ambao wanaweza kuchukua hatua ya kumuua yule mtoto kwa sababu amemchafua
bosi wao.”
PILI; Sura ya pili ambayo imeangaliwa kuhusu hatari ya maisha ya
denti huyo ni kwamba Kapuya anao maadui wa kisiasa ambao wanaweza
kutumia mgogoro huo kujifaidisha.
Laura
Kamugisha aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook: “Kuna sayansi moja
hapa, adui wa Kapuya anaweza kumuwinda huyo mwanafunzi na kumuua ili
kuzidi kumuweka Kapuya matatani.
“Leo ikitokea huyo mwanafunzi ameuawa, kila mmoja fikra zake
zitaelekezwa kwa Kapuya. Kwa kweli huyu mtoto yupo hatarini, inawezekana
Kapuya akampuuza lakini maadui zake wakamuua ili kumkomoa. Mwanafunzi
akiuawa, Kapuya atapelekwa mahabusu na baadaye mahakamani.”
SHAHIDI MUHIMU AZUNGUMZA NA RISASI JUMAMOSI
Mrembo (jina tunalo) ambaye ni rafiki wa denti anayedai kubakwa,
alisema kuwa ameshangaa kusikia suala hilo limefika kwenye vyombo vya
habari kwa sababu huko nyuma yeye alishalisimamia na mambo yakaisha.
“Sijui kuhusu
kubakwa, ila … (anataja jina la denti) aliniambia madai yake,
nikampeleka kwa mheshimiwa, kusema kweli nilimbana mheshimiwa na fedha
zilitoka. Mimi mwenyewe nilipata mgao,” alisema mrembo huyo.
Akaongeza: “Ninavyojua walikubaliana, siyo kubakwa. Na mimi
nilimsaidia kumbana mheshimiwa ili ampe pesa. Alikuwa anahitaji pesa ya
kwenda kulipa ada shuleni, pesa alipewa.
“Nilianza
kuwa mbali naye baada ya kuona amekuwa karibu na wanaharakati. Kuanzia
hapo hakunishirikisha kitu, japo tunawasiliana. Hata leo nimeongea naye,
ameniambia yupo… (anataja eneo moja, nje ya Dar).
“Kingine
ni kwamba wakati namsaidia ishu yake na mheshimiwa alikuwa anasoma
Mugabe Sekondari, sijui Turiani alihamia lini. Na kuhusu Ukimwi mimi
sijui hilo, ila natambua kwamba yule mwanafunzi anatumia dawa.
“Hapa lazima niwe mkweli, siwezi kuthibitisha kama kweli ni Ukimwi na kama ni kweli aliyemwambukiza simjui,” alisema.
KAPUYA VIPI?
Juzi, mwandishi wetu
alijitahidi kwa kila namna kumpata Kapuya kupitia simu zake tatu za
mkononi, mbili za Airtel na moja ya Vodacom lakini hakupatikana.
Mbili hazikuwa zikipatikana
lakini moja ilikuwa ikiita bila kupokelewa, ingawa wakati mwingine
ilipopigwa ilionesha mwenye simu alikuwa akizungumza, hivyo kuonesha
hakutaka kuwasiliana na mwandishi wetu.
Pamoja na kutumiwa SMS
inayomuuliza kuhusu tuhuma hizo, bado Kapuya ambaye kwa sasa ni Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, hakutoa
ushirikiano.
No comments:
Post a Comment