Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Tuesday, October 8, 2013

MANENO MAZITOOO....!! DIAMOND AKANUSHA KURUDIANA NA WEMA SEPETU NA KUZUNGUMZIA KUVUJA KWA WIMBO WA NIKIFA KESHO CHECK HAPA.

Baada ya minong’ono mingi iliyosambaa kwenye magazeti ya udaku kuwa Diamond na Wema Sepetu wamerudiana tena, hitmaker huyo wa Number One, ameamua kufunguka na kuusema ukweli.
Kupitia Facebook, Diamond amesema habari hizo si za kweli na kwamba yeye na Penny bado wapo pamoja na mapenzi pomoni.
“Uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye account yangu ya Instagram. Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya mapenzi basi msizungumze ama kushiriki kwa chochote,” amehoji Diamond kwenye maelezo aliyoyaweka Facebook.
“Futeni huo uzamani na mbadilike, ina maana mnapenda kuona watu wanauadui… ni muda wa kufanya kazi ili kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo na faida.”
 
Alimalizia kwa ujumbe mzito na kwa herufi kubwa, “I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA.”
Katika hatua nyingine wakati wimbo mpya ‘My Number One’ ukiwa unaendelea kufanya vizuri katika chati mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, wiki hii kuna wimbo wake mwingine unaitwa ‘Nikifa Kesho’ umevuja na kusambaa kimya kimya kwenye mitandao.
Sio mara ya kwanza kwa nyimbo za Diamond kuvuja lakini sababu ya kuvuja kwa wimbo huu wa sasa ‘Nikifa Kesho’ iliyotolewa na Platnumz ni hii,
“Kuvujisha Nyimbo yangu hakuwezi kunipunguzia wala Kunidhuru chochote… Sanasana utanizidishia Umaarufu na kunipa Show zaidi… Kama nimeacha kurecord nyimbo Studio kwako Uspanick, Relax.. tafta Msanii mwingine Mkali zaidi yangu umrecordie Ngoma Ahit kushinda mimi….ila Kuvujisha Unajisumbua bure!”. ameandika ujumbe huo muda mfupi uliopita Kupitia instagram.
Pamoja kuwa hajatajwa kwa jina, lakini producer ambaye amekua akifanya naye kazi kwa muda mrefu kipindi kilichopita ni Manecky wa A.M Records, na hit song yake ya sasa ‘Number One’ ameifanya kwa Sheddy Clever, hivyo ‘kuna uwezekano mkubwa’ producer anayezungumziwa katika ujumbe huo ni Manecky!!

No comments:

Post a Comment