Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Rehema Nchimbi, Kaimu kamanda wa
polisi Mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda na kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma
mjini Ester Mgongolwa wakienda kupokea maandamano yaliyofanyika siku ya
usalama Barabarani.
Askali wa Jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] wakiongoza
maandamano ya siku ya usalama Barabarani yaliyofanyika juzi mkoani
Dodoma
Waendesha Bodaboda mjini Dodoma wakiandamana katika
maandamano ya amani yaliyoanzia kitio cha polisi kati kuelekea viwanja
vya barafu wakati wa maadhimisho ya usalama barabarani
Kipima Ulevi kitakachotumika na polisi wa usalama
Barabarani kuwagundua madereva wanaoendesha vyombo vya usafili huku
wakiwa wamelewa.
Na John Banda, Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka madereva
wa magari ya Abiria na mizigo wanaopitia
mkoa huo kuacha kutumia kilevi chochote ikiwemo viroba wanapokuwa Barabarani la
sivyo kufutiwa Leseni zao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauri hiyo siku ya usalama
Barabarani iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma juzi.
Nchimbi alisema ulevi kwa madereva hao umekuwa
ukiwasababishia kuwa wazembe barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha magali ya
abiria kwa maana ya mabasi na maroli ya mizigo na huwa ni chanzo cha ajali za
mara kwa mara.
Dr huyo wa Farsafa alisema ana taarifa za kutosha za ulevi
kwa baadhi ya madereva hao na hivyo atatumia jeshi la polisi kuwanasa na
kuwafutia leseni zao.
Aliongeza kuwa mbinu watakayotumia jeshi la polisi ni
kuwapima madereva wote wanaoingia na kutoka ndani ya mkoa wa Dodoma kwa kipimo maalumu cha kung’amua ulevi na
atakaegundulika kuendesha akiwa amekunywa pombe au aina yoyote ya kilevi
ikiwemo viroba atafutiwa leseni.
‘’Hivi sasa mkoa wetu unapoelekea kuwa jiji tunatakiwa pia
kuwa mfano wa kuigwa na mikoa mingine kuhusu udhibiti wa madereva walevi, hivyo
Dereva yoyote ili awe salama ahakikishe hajihusishi na ulevi ili aweze kupita
mkoa huu akiwa salama la sivyo apitie juu ama kama kuna njia ya kuzunguka apite
huko’’, alisema Dr. Chimbi
Aidha alisema zoezi hilo la kupima madereva walevi litaanzia
kwa wale wa Daladala na Bodaboda ambao wamekuwa wakinyonya viroba hata
wanapokuwa wanaendesha abiria wao bila kujali, aliwaagiza polisi kufavamia
maeneo yote wanakopakilia na kuhakikisha wanawapima hapo hapo na atakaebainika
uzi ni uleule wa kufutiwa leseni.
No comments:
Post a Comment