Na Cresensia Kapinga,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na Askari wa
kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini
wamewakamata watu watatu wakazi wa kitongoji cha Mamilamba kilichopo
kijiji cha Ligunga wilayani Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na pembe za ndovu 23 zenye uzito kilo 58.75 yenye thmani za Tsh 510,080,000.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana mchana ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deus Dedit Nsimeke amesema kuwa matukio hayo ni mwendelezo wa ukamataji wa meno ya tembo mikia na nyara zingine na nimfululizo wa matukio mengi wa ukamataji wa nyara za serikali ambao unafanywa kwa kushirikiana na jeshi la polisi ,kikosi cha kuzuia ujangili pamoja na wananchi wa maeneo husika.
Amesema, katika tukio la kwanza ambalo lilitokea juzi majira ya saaa mbili asubuhi huko katika eneo la kijiji cha ligunga,Askari polisi pamoja na askari wa wanayama pori wakiwa kwenye doria walimkamata Yasin Mbweso (31) mkazi wa kijiji hicho akiwa na pembe za ndovu 22 zenye uzito wa kilo gram 58.75,vipande saba vya nyama ya nyati ,pamoja na miguu miwili ya nyati, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 267,040,000.
Amefafanunua kuwa ,Yasin Mbweso maarufu kwa jina la Omary pia alikamatwa akiwa na mizani moja ya kupimia meno ya ndovu ambapo vitu hivyo vyote alikutwa navyo akiwa amehifadhi uvunguni mwa kitanda ndani ya nyumba yake na alipohojiwa katika mahojiano ya awali na polisi mtuhumiwa alikiri na kusema kuwa chanzo ni Kipato.
Amelitaja tukio lingine kuwa ni lilitokea juzi majira ya saa 2.30 usiku huko katika kijiji cha Ligunga ambako asakari polisi wakiwa na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini ambao walikuwa doria walifanikiwa kuwakamata watu wawili ambao aliwataja kuwa ni Rashidi Msinga (18) na Said Abdalah (17) wote wakazi wa kitongiji cha Namilamba kilichopo katika kijiji cha Ligunga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa na jino moja la Tembi,Mikia 10 ya Tembo pamoja na vipande vitatu vya nyama ya nyati vyote vikiwa na thamani ya sh 243,040,000. Pamoja na mizani moja ya kupimia meno ya tembo.
Aidha kamanda Nsimeki alilitaja tukio lingine kuwa lilitokea juzi majira ya saa 9 alasili huko katika kitongoji cha namilamba kijiji cha Ligunga ambako Yasini Mbweso (22) alikutwa akiwa na bunduki moja aina ya Liffle yenye namba za usajiri 458 akiwa namiliki bila kibali ambayo ilikutwa ikiwa imehifadhiwa kwenye dari ya nyumba yake ya nyasi.
Hata hivyo amewataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pamoja na kikosi cha kuzuia ujangiri kanda ya kusini na wananchi watakao fanikisha kukamatwa kwa majangiri watapewa donge nono la sh.milioni 2 kwa yeyote atakayefanikisha kuwanasa majangiri.
No comments:
Post a Comment