Chama
cha Mapinduzi(CCM) kimesisitiza kuwa bado mfumo wa sasa wa serikali
mbili ndio mfumo muafaka licha ya kuwapo changamoto mbalimbali zilizopo
na hivyo kuwa na serikali tatu ni kujiongezea mzigo bila ya sababu
yoyote.
Katibu
wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema hayo jijini Dar es salaam
alipokuwa akizungumza katika mjadala wa mchakato wa katiba mpya ambao
umeshirikisha vijana wa CCM toka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es salaam.
Naye
Mh. Stepheni Wasira ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mahusinao na
Uratibu amesema kuwa vijana ndio walinzi wa maadili ya nchi na hivyo
lazima washiriki vyema katika mchakato wa katiba unaoendelea sasa.
CHANZO: ITV
No comments:
Post a Comment