Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Sunday, July 28, 2013

MICHUANO YA CHAN YAPAMBA MOTO



Timu ya taifa ya Nogeria
Timu saba tayari zimejikatia tikiti ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi nyumbani itakayoandaliwa nchini Afrika Kusini mwaka ujao.
Nigeria imeonekana kujikatia tikiti baada ya kuilaza Ivory Coast 4-1 katika mechi ya awamu ya kwanza.
Ikiwa Nigeria itashinda mechi ya marudiano, basi itakuwa imejihakikishia nafasi katika fainali hizo.
Baada ya kuondolewa katika fainali zilizopita na Ghana na Niger, Super Eagles ya Nigeria inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kumaliza ukame wa miaka mitano wa kutoshiriki katika fainali hizo.
Kocha wa timu hiyo Stephen Keshi amesema watajiandaa vyema kwa mechi hiyo kwa kuwa itakuwa jambo la kushangaza ikiwa watapoteza mechi hiyon ya awamu ya pili.
Hata hivyo Ivory coast itakuwa na kibarua kigumu kwa kuwa wachezaji wake watatu walipewa kadi nyekundu.
Ethiopia ni nchi nyingine ambayp inatarajia kujikatia tikiti ya fainlai hizo kwa mara kwanza.


Shabiki wa DRC
Ethiopia iliilaza Rwanda kwa bao moja kwa bila mjini Adis Ababa.
Baaday ya kuilaza Tanzania kwa bao moja kwa bila Uganda kwa mara nyingine tena huenda ikafuzu kwa fainali hizo ikiwa itaibuka na ushindi katika mechi ya raundi ya pili.
Lakini Uganda Crane imewahi kupoteza nafasi kama hiyo wakati wa mechi yao ya mwisho na kocha wa Uganda Milutin Micho Sredojevic ana wasi wasi sana kuhusiana na wapinzani wao Taifa Stars.
Mali in anafasi nzuri baada ya kuilaza Guinea 3-1 katika mechi ya awamu ya kwaza sawia na Sudan ambayo ilitoka sare 1-1 na Burundi.
Lakini Burkina Faso na mabingwa wa kombe hilo mwaka wa 2009 Jamuhuri ya Kidewmokrasia ya Congo wanakibarua kigumu katika mechi zao za mwisho dhidi ya Niger na Congo Brazzaville mtawalia.

No comments:

Post a Comment