
Wapiganaji walioko katika eneo la Delta hutekeleza visa vya utekaji nyara mara kwa mara
Serikali ya Nigeria
imesema kuwa mamake waziri wa fedha , Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye
alikuwa ametekwa nyara kutoka nyumbani kwake katika jimbo la Delta siku
tano zilzopita ameachiliwa.
Gavana wa jimbo la Delta (Emmanuel Uduaghan)
ameimabia BBC kuwa Kamene Okonjo aliachiliwa bila fujo yoyote na hakuna
fedha za ukombozi zilizolipwa ili aachiliwe.Kwa sasa haijulikani ikiwa walitoa kikombozi kabla ya kuachiliwa kwa mamake waziri huyo.
Gavana wa jimbo hilo alisema kuwa sio sera ya serikali kulipa kikombozi ili kuachiliwa kwa mateka lakini wakati mwingine familia huzungumza na wapiganaji hao kwa faragha kuona ikiwa wanaweza kuwaachilia jamaa zao.
''Kwa upande wetu sisi hatukusema chochote kuhusu kikombozi na wala hatukukubali kulipa wala kushauriana na watekaji nyara kuhusu kuwalipa,'' alisema gavana huyo.
Mwanamume aliyemleta nyumbani Bi Okonjo kwa sasa amekamatwa na polisi na anahojiwa kuhusu yaliyojiri.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara nchini Nigeria na wala taarifa hizo huwa hazigongi vyombo vya habari.
Wafanyabiashara, wacheza soka, na wasomi wamekuwa wakitekwa nyara huku watekaji wao wakidai kikombozi katika maeneo ya Kusini katika siku za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment