Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Monday, March 10, 2014

WANAFUNZI WA CBE DODOMA WADUMISHA MAHUSIANO NDANI YA JAMII INAYOWAZUNGUKA.

     Rais wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma   Mh . Remidius  Mwema  Emmanuel   akiwa katika Eneo la  makole Tayari kushiriki zoezi la usafi katika Kata ya Makole Mkoani Dodoma.


Wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Dodoma chini ya Rais wao Mhe. Remidius Emmanuel  wamefanya  usafi katika kata ya  Makole. 
Akizungumza na  dhumuni la tukio hilo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mhe. Remidius  amesema  wameamua kufanya  Usafi kama sehemu ya  kudumisha mahusiano  na jamii zinazokizunguka chuo hicho. Ingawa  amepongeza kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa Marais wa vyuo  vya Dodoma ambao wameweza kushiriki katika zoezi hilo. Akiwatambua kwa majina , Amesema   Marais hao ni pamoja na  ,Mhe  Mahamudu Rashidi Hussein  (Makamu wa Rais  UDOM) , Bernard Janus ( College of Social Sciences) , Kagombora Joanes   (College of  Earth Sciences)  na Mhe. Katumbi Edmund J. Rais wa Chuo kikuu cha ST. John Tanzania.

Katika hatua nyingine Viongozi hao wamekemea  vikali tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya majina ya Vyuo vyao  kwa nia ya kujipatia umaarufu ikiwa ni pamoja na   kujenga dhana potofu  dhidi ya Maadili  ya wanafunzi wa vyuo  vyao. Akizungumza kwa uchungu mkubwa Rais wa  CBE Mhe Remidius  amesema   Baadhi ya wamiliki wa Blog  wamekuwa  na tabia ya kutumia picha  chafu  kutoka mataifa mbalimbali  na kisha   kuandika  kuwa ni wanafunzi wa vyuo  vikuu , " Lazima ifike hatua  ifahamike  kwamba   Blogu  zina heshima yake na wapo watu wanaendesha   maisha  yao kupitia  Blogu zao, hivyo nawaomba watu wachache  wanao tumia  Blogu zao vibaya  kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanaondoa dhana  ya uwepo  wa Blogu hizo" Alisema  Rais huyo.

Kwa upande wake Rais wa St. John Mhe Katumbi   Ameitaka jamii pia  kuyazungumzia  mazuri yanayofanywa na vyuo hivyo  na sio kuwa  na mtizamo hasi na dhidi ya vyuo  vikuu  pamoja na taasisi za Elimu ya juu.

 
 Baadhi ya Wanafunzi  wa CBE  pamoja na Ma -rais  wa vyuo vya Dodoma  wa kielekea katika eneo jingine tayari kuendelea na zoezi la usafi.
Hali  ilikuwa hivi  wakati Wanafunzi  wakiendelea na zoezi la kufanya usafi
Rais  UDOM (college of Earth Sciences ) Bw. Kagombora Joanes  Akishiriki katika  usafi.
Spika wa Bunge la Wanafunzi  (CBE) Mh . Frank Mshana (Anayeruka) akiwa na Fyekeo  Mkononi tayari kuendelea  na shughuli  ya Usafi.
Rais wa  Chuo Kikuu cha St. John  Mhe. Katumbi Edmund . j.  Akishiriki katika zoezi hilo la Usafi  , lililo andaliwa na  Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE - Dodoma)
Makamu wa Rais wa Chuo kikuu cha  Dodoma  Mhe  Mahamudu Rashidi Hussein (Mkono wa Kulia)  akishiriki kikamilifu katika zoezi hilo  la kufanya usafi.
Wanafunzi hao wakihitimisha  zoezi hilo  kwa kukutana na  Uongozi wa kata ya Makole.

No comments:

Post a Comment