Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Monday, March 10, 2014

MA- RAIS WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU NA VYUO VIKUU VYA DODOMA WAFUNGUKA.......SOMA HAPA!

             Rais  wa Serikali ya  Wanafunzi Chuo  Cha CBE  Dodoma   Bw. Remidius Emmanuel

Marais wa  Taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu vya Dodoma  leo (09/03/2014)   wametoa yao ya moyoni   wakati wakishiriki kampeni ya kufanya usafi  iliyoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE -Dodoma.
Viongozi hao   wamesema  mara nyingi vyuo vyao vimekuwa vikitumika  visivyo katika jamii hatua inayopelekea  mtizamo hasi dhidi ya vyuo hivyo kutoka katika jamii na taifa kwa ujumla.
 Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi  ya CBE Mhe. Remidius Emmanuel  amesema  " Taaluma ya habari inapaswa kuheshimiwa na kila kada , wapo baadhi wa wamiliki  wachache  wa baadhi ya Blogu wamekuwa  wakitumia Blogu hizo kuchafua vyuo hivyo  hatua ambayo inaleta mtizamo hasi katika jamii,. Mfano Mwaka jana (2013)  ipo baadhi ya mitandao ya kijamii (Blogu)  ziliwaonyesha baadhi ya  vijana wakifanya vitendo vya ngono kwa ku- ect picha  hizo na kisha   waandishi wa habari hiyo walidai kuwa  vijana hao ni wa CBE kitu ambacho si kweli na hawakuwa vijana (wanafunzi)  wa CBE . Upotoshaji huo umekuwa ukileta madhara  kwa  chuo lakini pia  kuharibu  sifa na dhana   ya kukubalika kwa kiwango cha elimu katika vyuo vyetu. Aliongeza kwa kusema   Serikali inapaswa  kuweka  taratibu za  kuwachukulia hatua baadhi ya Wamiliki wa Blogu wanao  tia doa tasnia hiyo nyeti ya habari. Ikumbukwe kwamba  Blogu ni  chombo chenye heshima zake na watu wanaishi  na kuendesha maisha yao kupitia Blogu, hivyo sio vema watu wachache waharibu taswira ya   mitandao hiyo  ya kijamii kwa kupotosha  umma  na kujenga dhana potofu na mitazamo dhidi ya   uwepo wa Blogu hizo" Alisema  Rais huyo wa CBE Dodoma.
Makamu wa  Rais  Serikali ya  Wanafunzi Chuo  kikuu ca Dodoma    Bw.  Mahamudu  Rashid Hussein
Kwa upande wake ,Makamu wa  Rais  Serikali ya  Wanafunzi Chuo  kikuu ca Dodoma    Bw.  Mahamudu  Rashid Hussein   amesema ifike wakati  jamii  ijenge tabia ya   kuyazungumzia na  mazuri yanayofanywa na  vyuo /wanavyuo  badala ya kujikita katika mlengo wa   kuvichafua vyuo na taaluma yake. Amesema  , Hakuna chuo ambacho  kinaunga mkono  ukiukwaji wa maadili kwani kila chuo kinazo taratibu na sheria zake za   kulinda  Maadili ya chuo husika. Lakini inapotokea   mtu akaamua   kutumia jina la chuo katika mtizamo hasi kwa maana ya  kujipatia idadi kubwa ya watu wanaotembelea   Mitandao ya kijamii (Blogu)  au kwa maana ya kuuza sana magazeti kwa habari ambazo hazina ukweli  ni kupotosha jamii na  kuharibu sifa za vyuo. Ni vema  taaluma ya habari ikaendelea kulindwa  kwa  kutoa habari yenye ulinganifu (Ku - Balance habari)  na  ukweli  kutoa vyanzo  fasaha. "Sio mtu  anapiga/kuchukua picha  chafu  katika mitandao  alafu anasema ni  wanafunzi wa vyuo "Alisema  Rais huyo .
      Rais  wa Serikali ya  Wanafunzi Chuo  St. John    Bw. Katumbi  Edmund  J. Akizungumza na Vyombo vya Habari.
Katika hatua nyingine Rais wa Chuo kikuu cha St. John  Mhe Katumbi  Edmund  J. amesema   vyuo  vikuu  vitaendelea kutoa huduma  mbalimbali katika jamii  na kuongeza  kuwa  ni vema jamii ikaendelea kutoa ushirikiano  pale wanavyuo wanaposhiriki katika huduma za kijamii. 
Bw. Katumbi  amesema anashangazwa na dhana  ya kwamba wanafunzi wa vyuo wamekuwa wakijiuza    kwa Tsh. 500, Amesema  hiyo ni fedheha  na aingii akilini kwa mwanachuo ambaye analipa  Mamilioni ya fedha  katika Elimu yake  alafu aende  akajiuze kwa Tsh 500 hizi ni dhana potofu za uongo ambazo  hazipaswi kuvumiliwa.
"Nashangaa kwa nini mambo mazuri    hayaandikwi  na badala yake   tumekuwa tukiandikwa  na kusomeka katika mtizamo hasi  kwenye  jamii, hivyo niiombe  jamii   iwachukulie wanavyuo kama  watu  wenye nia njema   na  wako tayari kushirikiana na jamii husika  katika  kuzitumia taaluma zao kuleta maendeleo  ya kiuchumi na kijamii.

No comments:

Post a Comment