Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Saturday, December 14, 2013

MANDERA KUZIKWA KIJIJINI KWAKE QUNU.

Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 14 desemba 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Jumapili 15 desemba 2013

Kijiji cha Qunu, nyumbani kwa Hayati Nelson Mandela
Mazishi ya rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini Mzee Nelson mandela aliyefariki juma moja lililopita, yanafanyika baadaye leo kijijini kwake Qunu ambapo watu mbalimbali ambao wamewasili kwa mazishi haya wanamuelezea Mandela kama kiongozi aliyelelewa pia kwa misingi ya kijadi.
Wananchi wengi walitamani kutoa heshima za mwisho na hata kukesha eneo hilo lakini wengine walikosa nafasi kutokana na umati kuwa mkubwa zaidi.
Mwili wa Hayati Madiba utapelekwa kijijini kwake Qunu hii leo tayari kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho jumapili.
Wakati huo huo serikali ya Afrika Kusini imesema inachunguza ili kubaini waliohusika kumuajiri Mkalimani wa lugha za alama ambaye alilalamikiwa kupotosha kwa kutumia ishara zisizo sahihi katika kumbukumbu ya kumuenzi Mandela iliyofanyika siku ya jumanne.
Mkalimani huyo Thamsanqa Jantjie alitumika kutafrisi hotuba za viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Rais wa Marekani Barack Obama.
Hivi karibuni mtu huyo alijitokeza mbele ya wanahabari na kuomba radhi kuwa hakufanya kazi yake kwa umahiri kutokana na kukabiliwa na maradhi lakini yeye ni mtaalamu wa kazi hiyo.
Kituo kimoja cha Televisheni cha binafsi nchini humo cha eNCA kimeripoti kuwa mtu huyo amewahi kukabiliwa na mashtaka ya jinai yakiwemo mauaji na utekaji.
Msemaji wa serikali Phumla Williams amesema serikali inachunguza iwapo makosa ya kiusalama yalifanyika hadi Jantjie akapewa pasi za usalama.

No comments:

Post a Comment