Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Wednesday, November 20, 2013

MANENO YA MFALME SELE; BILA HELA AU KUJIPENDEKEZA, WATANGAZAJI WENGI HAWACHEZI NGOMA YAKO




Afande Sele amesema baadhi ya watangazaji wa radio nchini hucheza nyimbo za wasanii aidha kwa kupewa hela mara kwa mara ama kwa wasanii wasanii kujipendekeza kwao.
Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi juzi, Afande amesema hiyo ndio sababu kubwa inayowafanya wasanii wengi wa zamani wapoteze umaarufu.
“Inakuwa kitu cha ajabu kusikia dogo katoka shule juzi kapata kazi radio fulani naye anajiona yupo top anaanza kukuletea pozi. Hata kama usipompa hela katika wiki, anataka umpigie simu mara tatu, au utafute muda uende anapofanya kazi ufike uanze ‘vipi mwana, inakuaje mwana, niambie mwana’ kumpa mashavu kumfagilia, ndio inavyokuwa,” alisema Afande.
Katika hatua nyingine Afande alisema hajawahi kutokea producer anayemkubali zaidi ya P-Funk Majani.

No comments:

Post a Comment