Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, August 22, 2013

MENEJA WA OMMY DIMPOZ AELEKEZA NGUVU ZAKE KWA P SQUARE!

MENEJA wa Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Mbarouk Issa ‘Mubenga’ amesema lengo la msanii huyo hivi sasa ni kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama P Square na wengine ambao wanafanya vizuri.
Kwa mujibu wa Mubenga, Dimpoz ana malengo ya kuwa msanii mkubwa, hivyo anaomba sapoti ya kutosha kwa wapenzi wa kazi zake ili aweze kufikia hapo.
Alisema nia hiyo ya kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani, imekuja baada ya kuona anakubalika kila kona na kupata mialiko mbalimbali katika nchi za jirani.
“Wakati anaanza, Dimpoz alikuwa haamini kama anaweza akakubalika kama sasa hivi, kiukweli anafanya vizuri sana sio hapa Tanzania tu, hata nchi za jirani wanamkubali sana,” alisema.
Mbali na hilo, msanii huyo ana mpango wa kufungua kampuni yake ambayo itakuwa inahusisha shughuli mbalimbali za muziki na mambo mengine.
Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Tupogo’, alichoimba na mkali kutoka Nigeria, JMartin na alishawahi kung’ara na kazi nyingine kama ‘Nai Nai’, ‘Baadae’ na ‘Me and You’, ambavyo vilimtambulisha vema na kufanya vizuri katika soko la muziki.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment