Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Thursday, March 27, 2014

RAIS APONGEZWA NA NAIBU WAZIRI WA MADINI KWAKUWA MBUNIFU KATIKA SERIKALI YAKE.

   Naibu waziri wa  Madini Mhe. Steven Masele
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Steven Masele  Amempongeza Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa  CBE Dodoma  kwa ubunifu wake  wa kuanzisha   Mashindano ya Remidius CUP . Waziri huyo amesema hayo jana baada ya kukutana  na  kufanya mazungumzo na Rais huyo   jana (25/03/2014) katika  ofisi yake  Mkoani Dodoma.
Katika hatua nyingine  Naibu waziri huyo amemtaka Rais huyo kuendelea kuwa mbunifu katika masuala mbalimbali yanayolenga kuwaletea maendeleo  wanafunzi wake anaowaongoza  na jamii  nzima kwa ujumla ili kuondoa dhana potofu ambazo  zimekuwa  zikiibuliwa  dhidi  ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo kukiuka maadili.
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi  CBE Mhe. Remidius  Amemshukuru  kiongozi huyo kwa kuahidi  ushirikiano  na kumpongeza kwa utayari wake wa  kuunga mkono juhudi za Vijana  hususani wasomi wa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu.

No comments:

Post a Comment