Pages

Ads 468x60px

LIKE THIS PAGE FIRST.

Friday, February 14, 2014

HII NDIO HISTORIA YA VALENTINE DAY


Historia ya siku ya valentine imetokana na Mtakatifu, Mchungaji/Askofu wa Kanisa katoliki wa miaka ya 496 baada ya Kristo ambaye aliitwa Valentine. Wengine wanamtaja kama Askofu wa kiprotestanti wakati wengine wakimtaja kama  Mtakatifu Padre/Askofu wa Kikatoliki ambao kwa pamoja wana historia iliyofanana. Hata ndani ya Katoliki bado kulikuwa na kutofautiana kwa kumfananisha na kuhani wa huko Roma na askofu wa Temin na wa tatu ni Mchungaji wa Kiprotestanti ambaye taarifa zake hazijulikani ila inaaminika aliishia Afrika katika utumishi wake.

Katika kipindi hicho Papa Gelasius alidhamiria kumuenzi Valentine kwa kuweka siku ya 14 Februari kama siku ya wapendanao duniani.

Historia inaeleza kuwa Askofu Valentine alikuwa akifundisha na kufungisha ndoa za siri kwa vijana wadogo wapendanao ambao walipigwa marufuku kuoana katika sheria za kirumi wakati huo kwa sababu walikuwa bado ni wadogo. Vile vile awakutakiwa kuoa kwa sababu wengi wao walikuwa ni maaskari na iliaminika kuwa askari mzuri na mkakamavu ni yule ambaye ajaoa.

Kwa sababu Valentine alikirimiwa na Mwenyezi Mungu karama za uponyaji, afisa mmoja wa magereza ambaye binti yake alikuwa ni kipofu aliposikia uwezo uliwekwa kwa Askofu Valentine ya uponyaji, alimwendea na kumuomba amponye binti yake apate kuona tena. Valentine alifanya hivyo kwa nguvu za Kimungu na binti huyo akapona na tangu hapo binti wa afisa wa magereza alimpenda Askofu Valentine na wakawa marafiki wa karibu.

Dola ya kirumi iligundua kuwa Valentine alikuwa akifundisha na kufungisha ndoa kwa vijana ambao bado ni wadogo kinyume na sheria za kirumi ambayo ilikataza vijana wadogo kuoa au kuolewa mpaka wawe wakubwa, dola ya kirumi ilimkamata na kumweka ndani mpaka hukumu yake itolewe.


Alihukumiwa kifo baadaye na muda mfupi kabla ya hukumu ya kifo kutekelezwa alimuomba kalamu na karatasi afisa wa magereza na kuandika barua ya kuagana kwenda kwa binti wa afisa wa magereza, maandishi ambayo yanaishi mpaka leo. Barua hiyo ndio inaaminika kuwa kadi ya kwanza ya valentine.

Baadaye valentine mwingine alitokea akampenda binti wa afisa wa magereza lakini maelezo yake haikupewa umuhimu na wanahistoria. Kwa hiyo tarehe 14 Februari kila mwaka ikawa ni siku ya wapendanao duniani. Lakini siku hii ilikuja kuwekwa rasmi kuanzia karne ya 14.

Siku ya valentine ilikuwa kwa umaarufu na ukubwa na katika miaka ya hivi karibuni iligeuka na kuwa ya kibiashara zaidi kwa kuuza kadi nyingi za valentine.
Ukweli Kuhusu Siku Valentine, Tarehe 14 Februari
Zaidi ya kadi milioni 1 sawa na 25% ya kadi zote huuzwa nchini Marekani tu.

Siku ya valentine ni ya pili kwa ukubwa na umaarufu baada ya Krismasi
Siku ya valentine huazimishwa kila mwaka tarehe 14, Februari
Inakadiriwa kuwa zaidi ya kadi za valentine milioni 50 huuzwa duniani kote
Kadi za valentine kwa umuhimu: huuzwa zaidi kwa waalimu, watoto, wamama, wake, na wapendanao
Alama Mbalimbali za Kadi ya Valentine na Maana Zake

Moyo — Ni alama ya upendo, inamaanisha kutoa moyo wako kwa umpendae, moyo kuchomwa na malaika mdogo ni ishara kwamba ukimpa moyo wako umpendae tegemea hatari ya kukataliwa.

Malaika mdogo — huyu malaika mdogo kwa kingereza anaitwa Cupid ambaye ina asili na utamaduni katika dola ya rumi na ikiwa na maana ya mungu wa upendo. Inaaminika kuwa, yeyote aliyechomwa na huyu malaika (mungu wa upendo) hatakufa bali ataangukia katika mapenzi

Ua waridi — Waridi ni ua maarufu duniani kwa kupeana nyakati za sikukuu na yenye alama ya uzuri.

Ua waridi huja na rangi mbalimbali na zote zikiwa na maana tofauti.
Nyekundu: ni upendo au mapenzi,
Manjano: kwa ajili ya urafiki na uwazi,
Nyeupe: ikiwa na maana ya pendo la kweli na uwazi,
Pinki: ni rangi ya urafiki na wapendanao,
Nyeusi: inamaanisha kuagana kwa wapendanao
Zawadi Zinazotolewa pamoja na Kadi ya Valentine

Mara nyingi, kadi ya valentine inatumwa na zawadi. Ni vigumu kuandika hapa ni zawadi gani utatuma na kadi hii kwani inategemea sana mguso wa mtu binafsi , jinsia, sababu, majira nk.

No comments:

Post a Comment